Ndugu wanahabari, Hali ya usalama Mkoa wa Arusha katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa ni shwari mpaka hivi sasa na hakuna tukio lolote la kihalifu limeripotiwa wala mtu kukamatwa kuhusiana na zoezi hilo. Kwa mujibu wa ratiba zoezi hili lilikuwa likamilike kesho tarehe 14.10.2019 lakini limeongezewa muda hadi tarehe 17.10.2019 saa 12 jioni. Jeshi la Polisi mkoani hapa litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Mkoa wa Arusha na litafanya kazi bila kumuonea mtu na halitakuwa na upendeleo kwa chama chochote cha siasa. Askari wote wameelekezwa kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo katika zoezi hili. 
Hivyo nitumie fursa hii kuwahakikishia Wananchi wote wa Mkoa wa Arusha wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwani tumejipanga katika kuhakikisha usalama wao na mali zao. 
Aidha kwa mujibu wa ratiba tunategemea msimamizi wa uchaguzi kuwasilisha kwa OCD ratiba za mikutano ya kampeni tarehe 14.11.2019. Kampeni zitaanza rasmi tarehe 17.11.2019 hadi tarehe 23.11.2019. Uchaguzi utakua tarehe 24.11.2019 narudia tena tarehe za uchaguzi ni zile zile kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na hazijabadilika. 
Imetolewa naJonathan Shanna – ACP Kamanda wa Polisi – Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...