Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya
mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’
Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki
hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama
Barabara na Reli.
Mazungumzo
hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu
Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza
kunufaika kutoka katika Benki hiyo.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu
wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo
yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika
mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian
Infrastructure Investment Bank’ yaliyofayika
katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.
Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens
Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.
Makamu
wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya
pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb)
kulia, na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa.
Kulia kwa Mhe. Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe.
Mashimba Ndaki na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania, Prof. Florens Luoga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...