Na Mwandishi wetu,

Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, kundi la kwanza la watalii hao lililokuwa na zaidi ya watalii 200 wamewasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 mwezi Oktoba.

Kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya makampuni ya uwakala wa utalii kukamilisha taratibu za safari zao.

“Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi” Taarifa inasomeka.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kuwa, Tanzania imejipanga
kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini.

“Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda”. Taarifa inasomeka.

Mwezi Aprili 2019, Serikali ilipokea watalii 1,000 kutoka Israel. Aidha, mwezi Mei,2019 serikali pia ilipokea watalii 330 wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka jimbo la Zhejiang, China ambao waliwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, KIA. Watalii hao walikuwa ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 ambao wanatarajiwa kutembelea Tanzania mwaka huu 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...