Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi  Kemilembe Mutasa katika mkutano huo wa wataalamu kutoka nchi za SADC wamekua wakizishawishi nchi mwanachama kuridhia itifaki ya hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi  ya mifuko ya plastiki. 



Na Vero Ignatus, Arusha.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC ,wanaotekeleza mkakati wa SADC pamoja na programu ya Mazingira na Mabadiliko ya tabianchi, sambamba na sera ya mazingira ya mwaka 1997 pamoja na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.


Katika kutekeleza programu ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika SADC, ni pamoja na kuwajengea uwezo nchi wanachama kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,kubadilishana ujuzi wa uzoefu katika masuala ya kuhifadhi mazingira, na kufanya tafiti katika vyuo vikuu ili kupata suluhisho la changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi.



Hata hivyo Wataalaalamu wa mazingira kutoka Tanzania, wanaoshiriki mkutano wa Mawaziri wa,Maliasili na Utalii wameaswa kuanza juhudi za kuzishawishi nchi hizo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ili kudhibiti uharibifu wa mazingira katika ukanda huo.

Akizungumza mara baada ya kuhudhuria mkutano wa wataalamu wa maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii kwa nchi za SADC, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi  Kemilembe Mutasa alisema katika mkutano huo wa wataalamu kutoka nchi za SADC wamekua wakizishawishi nchi mwanachama kuridhia itifaki ya hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi  ya mifuko ya plastiki.

“Tanzania kuwa mwenyekiti wa SADC tunatumia fursa ya kushawishi nchi mwanachama kuhimiza agenda ya marufuku ya mifuko ya plastiki iweze kutolewa kwa nchi zote ikiwa ni mkakati wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Cletus Shengena alisema kuwa wataalamu wa mazingira kutoka nchi za SADC wamekua na mikutano ya kuweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiko ya tabia ya nchi ambayo ni changamoto kubwa inayokabili nchi wanachama  Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo.

Aidha Shengena alisema kuwa mkakati huo utawasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na athari ambazo zilizoanza kujitokeza ikiwemo mafuriko na upepo mkali na vimbunga katika nchi mwanachama.

Afisa Mazingira Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi.Emelda Teikwa Adam amesema kuwa wameangazia fursa za kukuza uchumi wa nchi za SADC kwa kutumia uchumi wa bluu unaojulikana kama uchumi wa bahari unaotumika kwa njia ya usafirishaji, uvuvi na kutoa nishati kwa maana ya uchimbaji wa mafuta na gesi kama njia za kukuza uchumi wa nchi za SADC.

Emelda alisema kuwa ili uchumi huo uwe endelevu mazingira yanapaswa kutunza na kulindwa ili wananchi waweze kunufaika na fursa za uchumi wa bluu ambao ukitumika vizuri unaweza kupunguza umasikini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...