Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Benson Security Systems na AfriTrack wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua mfumo wa kimtandao wa kudhibiti vyombo vya usafiri jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Teknolojia ambayo itakayotumia mtandao wa mawasiliano wa internet imezinduliwa na Kampuni ya Benson ya jijini Arusha ikishirikiana AfriTrack ya jijini Dar es Salaam yenye uwezo wa kuthibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto


Miqdaad Kassam ni Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Benson, amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa,kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana kwa kuwa itaonekana eneo iliyopo

“Ni teknolojia rahisi itakayodhibiti wizi wa pikipiki ambao sasa ni moja ya matatizo sugu yanayolalamikiwa na wateja wengi.Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu,”alisisitiza Kassam katika uzinduzi huo.

Salma Rothbletz ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja katika Kampuni hiyo,alisema kifaa hicho maalum hufungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja hupata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika siku yake.

Alifafanua kuwa mfumo huo hudhibiti udanganyifu wa madereva katika matumizi ya mafuta na umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki za kusafirisha abiria kufuatilia biashara yao kwa ukaribu na uhakika kwa kuwa wanaweza kujua kiasi cha mafuta kilichotumika kwa siku na hata umbali ambao pikipiki imetembea,” alifafanua.

Suhail Sheriff ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AfriTrack, amesema katika uzinduzi huo kuwa mtandao huo wa udhibiti wa vyombo vya usafiri unatumika pia katika malori na magari ya abiria na utasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa ajali za barabarani.

Amesema kuwa mfumo huo hudhibiti hali ya dereva kama yuko timamu kuendesha chombo husika na iwapo kuna dosari hutoa ishara ya tahadhari kwa dereva mwenyewe na mwenye gari kabla ya madhara yoyote, ikiwa ni pamoja na ajali, kutokea.

“Kama gari lina hitilafu za kiufundi au dereva ana tatizo lolote, mathalan la kiafya, mfumo hugundua na baada ya muda hutoa ishara ya tahadhari unaosaidia hatua za kuzuia madhara yatokanayo na hitilafu hiyo kuchukuliwa haraka,”alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Sheriff amesema kuwa vyombo vya usafiri vinapokuwa katika maeneo yasiyo na mtandao wa mawasiliano, ikiwa ni pamoja na porini na bahari kuu ambapo mawasiliano ni magumu,wanatumia mfumo wa mawasiliano wa setelaiti kufuatilia mwenendo wa vyombo hivyo katika maeneo hayo yasiyo na mtandao.

Aidha amesema kuwa mfumo huo tayari umeshaanza kwa mafanikio makubwa katika nchi za Ivory Coast, Malawi,Zambia na sasa umeingia nchini katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya

Kiure, Omar Kiure ni Mwakilishi wa Kampuni ya Uhandisi ya amesema katika uzinduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiri magari na madereva katika sekta ya usafirishaji ni ukombozi kutokana na kukithiri kwa wizi hasa wa mafuta unaosababisha hasara kubwa.

“Wizi wa mafuta katika katika sekta ya usafirishaji na ujenzi ni sehemu ya tatizo sugu na linalokera mno katika sekta ya ujenzi na kwa kweli mfumo huu utatusaidia kudhibiti wizi huu unaotutia hasara mno na kusababisha gharama kuwa juu,” alisema Kiure.

Athilyo Choga ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha amesema katika uzunduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiti utasaidia jeshi hilo kudhibiti na kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...