Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba kabudi amesema kuwa Mwalimu Julius Nyerere amegoma kufa na sisi tumegoma kuamini kama Mwalimu amekufa kutokana na hotuba zake kuishi kizazi hadi kizazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kabudi amesema kuwa mawazo ya Mwalimu yanaishi karne hadi karne.

" Mwalimu amefariki dunia ila amegoma kufa na amegoma kuacha kusimamia misingi ya nchi hii na sisi tumegoma kuamini kama amekufa na hiyo ni kupitia hotuba zake za muda mrefu ambazo zimekuwa zikiishi kila siku" ameeleza Prof. Kabudi.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kuthamini na kusimamia misingi aliyoiweka Mwalimu ili kuweza kulijenga taifa katika misingi ya maadili na kiitikadi.

"Tunu zinazotutambulisha ambazo Mwalimu alituachia lazima tuzitunze na hiyo ukiwepo muungano, haki, utu na usawa ili kuendelea kuliweka taifa letu katika nafasi njema zaidi" ameeleza.

Kuhusiana na lugha ya Kiswahili Prof. Kabudi amesema kuwa, lugha ya Kiswahili ni lugha ya ukombozi nchini na kusini mwa Afrika na nchi nyingi zimeeleza uhitaji wa walimu wa lugha hiyo nchini mwao hivyo amevitaka vyuo vinavyofundisha lugha ya Kiswahili kutumia nafasi hiyo katika kuieneza lugha hiyo ya ukombozi.

Amesema kuwa Chuo cha Dar es Salaam kimekuwa kikifundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni kutoka bara la Afrika kwa gharama sawa na wazawa,na kueleza kuwa jambo hilo ni jema na litasaidiakuipeleka mbele lugha adhimu ya Kiswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...