Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara,
Bi.Sekela Mwaisela akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kikao cha
Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya
biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia hotuba yaMkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.SekelaMwaisela, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara naKamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyikaJijini Dar es Salaam.

*****************************

Jumla ya vikwazo 174 sawa na asilimia 75 vimeondolewa ili kurahisisha ufanyajibiashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo sasaitawezesha kuwepo kwa biashara kubwa baina ya nchi hizo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Mkutano kati ya
Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.Sekela Mwaiselaalisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kanda zingine kuna sheriaambazo zinazingitia biashara.

“Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ibara ya 13(1) Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Biashara pamoja na Ibara ya 6 ya Itifaki ya Biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika (SADC) zinazitaka NchiWanachama kuondoa vikwazo vya zamani ili kuwezesha biashara kwawafanyabiashara”, Alisema Mwaisela.

Mwaisela alieleza kuwepo kwa juhudi za kuondoa kabisa vikwazo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikishirikisha kuwepo kwa vikao vya kamati za biashara, Mikutano ya Kikanda, Mikutano ya Mawaziri pamoja na Mikutano ya Nchi kwa Nchi hiyo itatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoa changamoto zao kwa utatuzi zaidi.

Katika kuteleza hilo Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wadau leo imefungua Mkutano wa wadau wa biashara ambapo agenda kubwa ni kuelimisha wafanyabiashara kuhusu kutoa taarifa iwapo watakutana na vikwazo mbalimbali wakiwa kwenye kusafirisha bidhaa zao.

“Kusudi kubwa la Mkutano huu leo ni kujadiliana kuhusu kutoa vikwazo lakini pia kuwawezesha wafanyabiashara kuwa na elimu kuhusu hivyo vikwazowanavyokutana navyo, sehemu gani ya kutoa taarifa kwa Msaada Zaidi”, alisema Mwaisela.

Alisema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kujenga miundombinu wezeshi ikiwemo Bandari, Reli, ambavyo vinaambana na ujenzi wa miradi mikubwa kama ule wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme Julias Nyerere Hydro Power Poject (JN HPP) ambao utazalisha Megawati 2,115.

Kwa upande wa wadau wa biashara wao wamesema kuwa Serikali imewezeshakuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara katika Jumuiya ya Nchi wanachama ukiachilia mbali kuwepo kwa vikwazo vidogovidogo ambavyo vinatatulika.

“Mkutano huu unaonesha nia njema ya Serikali kuweza kuwasiliana kwa karibu na wafanyabiashara ili kuweza kujua changamoto zao na mazingira ya biashara wanayokutana nayo sokoni, tumefurahi kwamba Serikali imejitahidi kupunguza changamoto za biashara” David Minja, Unilever.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...