WAANDISHI wa habari kutoka kanda zote nchini ambao wanahudumu katika redio za jamii, wameingia katika mafunzo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki watajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.
Akizungumza mjini hapa Christophe Legay, Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari ili waweze kuelimisha jamii.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya tatu kwa waandishi wa habari na yamegusa wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo hayo.
Legay alisema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabianchi majanga ya asili yamekuwa yakijitokeza sana na kwa kasi hivyo imeonekana haja ya kuwapatia wananchi mafunzo maalumu ya kukabiliana na majanga hayo ikiwa na pamoja na kujiweka tayari.

"Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia" alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.

Alisema kwa sasa wengi wa waandishi namna yao ya kuandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali.
Legay alisema watu wakitambua namna ya kusimamia maafa na matumizi ya raslimali na nyenzo za usimamizi hasara kwa mali na watu zitapungua.

Alisema pamoja na majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, pia kuna majanga yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile milipuko ya matanki, ajali mbalimbali ambazo wananchi amekuwa wakijihudumia badala ya kuokoa mali na watu.

Naye Kevin Robert, mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka UNESCO alisema ni wajibu wa waandishi wa habari kwanza kutambua namna ya kukabiliana na majanga, elimu ambayo itawapa undani wa nini kinatokea, wafanye nini na nani asaidie wawe na taarifa sahihi za kusaidia wananchi.

Robert alisema wanahabari hao kutoka Redio 25 na Mratibu kutoka mtandao wa Redio za Jamii zilizotawanyika nchini kote ikiwamo mikoa ya Lindi,Katavi, Kilimanjaro Mara wanafundishwa mifumo ya upashanaji habari katika maafa, mifumo ya habari, kitengo cha maafa na utaratibvu wake na namna nzuri ya kusaidia waliokumbwa na mafaa.

Tanzania kwa sasa imeshakabiliwa na majanga ya asili mengi kama  mafuriko, ukame, upepo mkali, tsunami, mmomonyoko wa bahari,  mvua za mawe na upepo mkali  kama wa Kahama na mafuriko ya Mtwara, 2015 na pia kulipuka kwa lori la mafuta mjini Morogoro.
Katika ajali ya Morogoro wananchi badala ya kuokoa walikuwa wanaiba mafuta hadi lori lilipolipuka.

Kevin aliwataka waandishi hao kutambua changamoto zilizopo pamoja na kuelewa Sheria ya Uratibu wa Misaada ya Maafa Namba 9 ya 1990 (iliyofutwa na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya 2015) na kujua kazi ya kitengo cha Kuratibu Misaada ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema ni matarajio ya UNESCO kuona kwamba mafunzo hayo yanaimarisha upashanaji habari wenye tija kubwa katika kukabili majanga na maafa.
 Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO, Christophe Legay akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Kevin Robert akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mratibu wa Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), Irene Makene akitoa salamu TADIO kwa waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Washiriki kutoka redio za jamii wakichangia maoni wakati wa mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Baadhi ya ya waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...