Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia vijana wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
Baadhi ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Sehemu ya viongozi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi. Katikati ni Katibu Mkuu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally.
Mama Gertrude Mongela akiwasilisha mada kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo uliofanyika Mkoani Lindi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mama Gertrude Mongela kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo. (Wa pili kutoka kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo huo wakifuatailia mada zilizokuwa zinawasilishwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba. (Wa pili kutoka Kushoto ni Mjukuu wa Mwalimu Julius Kambarage NyerereMjukuu wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bi. Ngusekera Nyerere akitoa salamu wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.
Wawasilishaji Mada wakisikiliza hoja zilizokuwa zikichangiwa na baadhi ya washiriki wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
Kijana mmoja wapo aliyeshiriki mdahalo huo akichangia mada kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuenzi na kuziishi fikra na mitazamo za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza umoja uliopo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Mkoani Lindi Oktoba 13, 2019, Waziri Mhagama alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake ili waendelee kujivunia juu ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.

“Vijana mna kila sababu ya kujivunia amani na umoja ulipo katika taifa letu kwa kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyewapenda watu wote bila kujali imani zao wala itikadi zao, alikuwa mzalendo na alitaka watanzania wote waishi kwa umoja,” alisema Mhagama.

Aidha alifafanua kuwa, Amani na umoja zilikuwa ni miongoni mwa tunu na falsafa kuu za Baba wa Taifa ambayo ndiyo matokeo ya umoja na mshikamano wa taifa uliopo sasa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo muhimu ambayo Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza katika kuwaunganisha watanzania ni pamoja na kulijengea uhuru taifa na watu watu wake, kudumisha amani, upendo, umoja, uzalendo, mshikamano na kuandaa sera za kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.

Pamoja na hayo alisisitiza pia vijana na wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuendeleza maono ya Baba wa Taifa ikiwemo mageuzi ya kiuchumi yenye manufaa kwa taifa.

Akitolea mfano sekta ya elimu ambayo serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa elimu bure ilikuwa ni falsafa ya Mwalimu katika kuwajenga watanzania fikra ya kujitegemea ili waweze kuukabili umasikini.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wananchi kuendeleza maudhui ya Mwenge wa uhuru ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha watanzania na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Mwalimu Julius Nyerere ataendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake aliojitolea katika kulijenga taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...