Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema sekta ya mifugo na uvuvi inachangia takribani asilimia 7.9 ya pato la Taifa.

Wazara hiyo imejipanga huku kuboresha sekta hiyo na kutarajia kufikia asilimia 10 hadi 25 ifikapo 2025 pamoja na uzalishaji wa malighafi katika sekta ya viwanda .

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wadau wa Sekta ya Mifugo wakiwemo wastaafu, Ole Gabriel amesema uboreshwaj kwa sekta hiyo kutafanya Tanzania kuwa ya viwanda na kuwafanya wafugaji kuwa na uchumi wa kati ikiwa ni kuchana na ufugaji wa mazoea.

Amesema ili kufikia lengo la kuongeza pato la taifa watanzania wanapaswa kupenda vitu vya ndani na kuhakikisha wananunua bidhaa za ngozi zinazotokana na mifugo hali ambayo italeta tija kwa nchi.

“Tatizo kubwa la Watanzania bado wanaumwa ugonjwa wa kununua vitu vya nje na sio ndani ya nchi wakiamini ndio bora wakati bidhaa zilizopo ni bora sana kwani uzalishaji madawa ya mifugo na vyakula vyake vinazalishwa hapa hapa nchini ”alisema Prof. Ole Gabriel

Aidha alisema Wastaafu waliofanya kazi katika sekta hiyo wanawajibu wa kuendelea kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika kutoa mafunzo mbalimbali katika vyuo vya mifugo ili mchango wao uendelee kuonekana katika jamii.

Prof. Ole Gabriel alisema katika mkutano huo watapata fursa ya kujadili mambo saba ikiwemo namna ya kuondoa vikwazo vya biashara ya mifugo ndani na nje ya nchi,kushauriana namna ya uboreshaji wa viwanda vya Mifugo,Namna ya kupata pembejeo za Mifugo kwa bei nafuu,Kudhibiti uingizaji wa mazao ya mifugo na mifugo ambayo zipo chini ya viwango na kujadili Mkakati wa uboreshaji wa Sekta ya mifugo.

Nae Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu amesema kuwa wanashirikiana na serikali vizuri kwa kuwaamini katika dawa.

Amesema kuwa Farm Base ni kampuni ya wazawa hivyo nia yao ni kuona wafugaji wanapata bidhaa bora katika kuendeleza sekta ya mifugo nchin.

“Wafugaji wengi wanafuga kwa mazoea wanaangalia bei ya kuuza na sio kuangalia bei ya gharama alizotumia katika utunzaji wa mifugo yake nah ii inawaangusha wafugaji wengi,”alisema Prof. Ole Gabriel

Kwa Upande wake Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt Mary Mashingo alisema wanaishukuru wizara hiyo kwa kuwakutanisha pamoja katika mkutano huo na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya mifugo.

“Mataifa mengi wazee waliostaafu katika sekta mbalimbali wamekuwa wanafanya kazi na kujitoa katika kutoa utaalamu wao huku wakijipangia muda wa kufanya kazi hizo,”alisema.
Bidhaa za Dawa zinazozalishwa na Farm Base wakionesha katika Mkutano Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Mstaafu  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dkt Mary Mashingo akitoa namna sekta ya mifugo inavyoweza kuwa na mchango kwa wafugaji kupata mikopo Benki ya TIB Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wastaafu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wa Mifugo wa Uvuvi katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu akizungumza namna wanavyoshirikiana serikali katika uzalishaji wa dawa za mifugo katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha  ya pamoja Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...