Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.

MSANII wa Muziki wa kizazi kipya miongoko ya mduara kutoka Zanzibar, Ally Ramadhani a.k.a  AT ametoa masikitiko yake kwa waandaaji wa matamasha na majukwaa kutoshirikishwa kwa wasanii wa kizanzibar.

AT amezungumza hayo leo na Ripota wetu katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JNCC, jijini Dar es salaam na nakueleza kuwa Sanaa yeyote ile ili ipanuke na kukua zaidi ni muhimu wasanii na wadau kushirikiana kwa pamoja na kutengeneza umoja ambao utaleta faida katika jamii na kupelekea sanaa kuimarika na kutangazika kimataifa.

"Tunatengwa sana hasa sisi wazanzibar kwani matamasha mengi hatushirikishwi wanajichagua wenyewe kwa wenyewe,"

Aidha, amewatoa hofu wasanii wachanga  kutokata tamaa katika vipaji vyao na kuvipigania .

"Nilikua na kipato duni sana ila nilijitahidi kununua nguo za mitumba ili ni shoot video zangu kwani niliamini mdogo mdogo ndio mwendo na hatimae nimefika hapa hivyo kwa wasanii wachanga watumie vitu ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi"

Aidha, AT ameeleza kuwa wasanii wasichoke kuwaomba wasanii waliotoboa kimuziki kuwasaidia kimawazo ili kuboresha kazi zao .

"Mimi nilikua msanii wa kwanza mchanga kumpandisha Alikiba kwenye daladala kutoka alipokua anaishi kariakoo hadi masaki kwa mtayarishaji wa Muziki Allen Mapigo nilijishusha na kumyenyekea kutokana na uhitaji wa Jambo likamilike,"

Hata hivyo amesema anajisikia faraja kuona bado ana nguvu na maono ya kuona ana nafasi ya kuwasaidia wasanii chipukizi wakike na kuwakuza kimuziki na kimaadili.

"Kwa Sasa wasanii wakike baadhi wamekua wakijiacha utupu ili tu wajulikane kwa haraka zaidi kutokana na kukosa nafasi wao wenyewe kupenya Kama wasanii wengine wakubwa walivopata nafasi,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...