Na Woinde Shizza,Arusha

Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji mhandisi Anton Sanga  amewataka mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha ( AUWSA) haraka iwezekanavyo kuhakikisha maji yanawafikia wakazi wa mji wa  Namanga wilayani Longido ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya maji kwa muda mrefu

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi katika chanzo cha maji cha mto simba kilichopo ndaniya hifadhi ya taifa ya Kinapa Naibu katibu amesema kuwa Ameridhishwa na ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji ambao ujenzi wake umeendana na thamani halisi ya fedha na umeshakamilika

Sanga Alisema kuwa maji yanayotoka katika chanzo hicho ni mengi ila bado hayawatoshelezi kwa muda mrefu kwani mradi huo ni wa miaka mitano hivyo waangalie uwezekano wa kuongeza uwezo wa maji hayo kuingia katika chanzo hicho ili yaweze kuwafikia wakazi wa mji wa namanga.

“nimewaagiza mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha waongee haraka iwezekanavyo watu wa bonde la pangani ambao wao ndio wanatoa huduma ya maji katika mikoa minne ambayo ni Tanga ,Kilimanjaro ,Arusha na manyara kuungana nao na kuangalia kama kunauwezekano maji haya yanayochukuliwa kutoka chanzo cha mto Simba kwenda Namanga yaongezewe kidogo ili yaweze kufika na kuwatosha wakazi wa mji wa Namanga”alisema Sanga

Aidha pia aliwataka AUWSA kuongeza kasi ya kuwaunganishia wateja wao maji kwa kasi na kwa haraka ili wananchi wote wa mji wa Namanga waweze kupata huduma hii ya maji kwa haraka na kwawakati.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justini Lijomba Amesema wamepokea maelekezo ili kufikisha maji hayo katika mji wa namanga hivyo watahakikisha maji hayo yanawafikia kwa wakati wakazi hao

Aidha alibainisha kuwa mradi huo umegarimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 15 na unatarajiwa kuhudumia kaya zoto za mji wa Namanga,alitumia muda huo kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kuwapa kipaumbele wakazi wa Namangan a Longido.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...