NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI inatarajia kutoa shilingi bilioni 3.200 kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Maji katika eneo la Ichemba wilayani Kaliua.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kukamilisha usanifu kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa hilo kwa gharama ya shilingi milioni 40.8 kwa kutumia mapato yake ya ndani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua ya kukagua miradi ya maji na kutatua kero za maji.

Alisema kukamilika kwa mradi huo utasaidia jumla ya wakazi 229,290 wa Kata za Ichemba, Kanoge, Mwongozo, Nhwande, Makingi, Sasu, Kanido, Milambo na Igombenkulu na wakimbizi kutoka Burundi.

Waziri huyo alisema ujenzi wa bwawa hilo unatarajiwa kuanza mara baada ya mvua za masika yam waka huu kumalizika.

Aidha Profesa Makame Mbarawa alisema kwa kutabua tatizo la maji katika eneo hilo , Serikali imetoa shilingi milioni 571 kwa ajili ya mradi wa dharura wa kutatua tatizo la maji Kaliua Mjini wakati wakisubiri utekeleza wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria.

Alisema mradi wa uletaji maji kutoka Ziwa Victoria katika mji wa Kaliua ni sehemu ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 ya Tanzania ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi triolioni 1.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema eneo hilo linakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji ardhini na kutokuwa na vyanzo vya kutosha vya maji.

Alisema msaada wa kuwasaidia wakazi wa Wilaya hiyo ni kupitia kujengewa mabwawa katika maeneo yenye uwezo wa kujengwa na kupata maji kutoka katika vyanzo kama vile Ziwa Victoria na mito iliyokaribu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...