Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (katikati) akimkabidhi Kamishna Mhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga moja ya kompyuta mpakato kati ya nne ambazo zimetolewa na Ubalozi wa China kwa ajili ya kusaidia katika mapambano dhidi ya Ujangili.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhi msaada wa runinga Kamishna Mhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga ambazo zitatumika kwa ajili ya kutolea elimu kwa njia ya video kwa wananchi wa kijiji cha Mhenda kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya Ujangili. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ya Taifa ya Mikumi, Mathew Mombona kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe.Adam Mgoi


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Wang Ke kabla ya kukabidhi vifaa vya ujangili pamoja pembejeo za kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Mhende wilayani Kilosa mkoani Morogoro.


Balozi wa China nchini Tanzania , Wang Ke akizungumza mara baada ya kukabidhi mbegu mbalimbali za mazao kwa Diwani wa Kata ya Mhe. Ali Athuman kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kujikita kwenye shughuli za kilimo na kuachana na vitendo vya ujangili.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang KE wakiwa kwenye pamoja na baaadhgi ya wananchi pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro.



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhende kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla ya kukabidhi Pembejeo za kilimo pamoja na vifaa vitakavyowasaidia Ulinzi shirikishi katika mapambano dhidi ya Ujangili.

Balozi wa China nchini Tanzania, WaNG KE akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhende kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kabla akiwaeleza wananchi kuwa Mabalozi kwa kujikita katika kilimo kwa kuendesha shughuli za kilimo kwa njia ya kisasa kwa kutumia mbegu za kisasa walizopewa na Ubalozi huo.

(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

……………………..
Ubalozi wa China nchini Tanzania umeunga juhudi za Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya ujangili kwa kuziwezesha jamii zinazoishi karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa kuzipa pembejeo za kilimo ikiwa pamoja na kuzijengea uwezo wa kulima kisasa ili kuwasaidia wananchi hao kuacha kujihusisha na vitendo vya ujangili.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati Ubalozi wa China nchini ukikabidhi msaada wa pembejeo za kilimo kwa wananchi wa kijiji cha Mhenda katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro

Ubalozi wa China nchini Tanzania umetoa msaada wa mbegu za mahindi yenye ujazo wa kilo 2500, mbegu za alizeti zenye ujazo wa kilo 150 pamoja mbegu za choroko zenye ujazo wa kilo 800

Mbali na msaada huo, Ubalozi huo umetoa jumla ya jozi 13 za sare za ulinzi shirikishi, buti 13, komputa mpakato nne pamoja runinga moja

Mhe.Kanyasu amesema lengo la vifaa hivyo ni kuwasaidia wananchi kujikita katika kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Kanyasu amesema vifaa hivyo vitatumika katika kutoa elimu kwa wananchi katika mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameipongeza Jamhuri ya watu wa China kukomesha soko la meno ya tembo na kuamua kutoa msaada kwa wanavijiji ili nao waweze kuachana na biashara hiyo haramu.

Awali, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amesema pembejeo za kilimo walizozitoa itakwenda sambamba na mafunzo yatakayotolewa na wataalam kutoka China watakaowafundisha wanakijiji kulima kwa kisasa ili waweze kuachana na vitendo vya ujangili.

Ameeleza kuwa Ubalozi wa China umeamua kuanza na kijiji hicho ili kuwasaidia wananchi kuweza kuzalisha mazao mengi ili wasiweze kujiingiza katika vitendo vya ujangili.

Amesema China imeamua kuisaidia Tanzania katika mapambano ya vita dhidi ya ujangilli kwa vile watalii wanakuja nchini kwa ajili ya kuangalia wanyama, hivyo vitendo vya ujangili vinakwamisha juhudi za serikali katika kujiletea maendeleo.

Aidha, Balozi huyo ameipongeza Taasisi ya Kova SUKOS Foundation inayoshughulikia majanga kwa kuratibu tukio hilo ikiwa pamoja na kujitoa kuhakikisha wananchi wa Mhende wanakabidhiwa misaada hiyo itakayowasaidia katika kujiondoa katika umasikini huku utalii ukizidi kushamiri.

Naye Diwani wa kata ya Mhenda, Ali Athumani amemshukuru Balozi wa China kwa msaada huo na kuahidi kuwa watakuwa mabalozi kwa vijiji vingine vilivyo karibu na Hifadhi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...