Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (kulia), jana akikabidhi moja ya mifuko 26 ya saruji kwa uongoziwa CCM Tawi la Katwe Buchosa Sengerema.Saruji hiyo yenye tahamni ya sh. 507,000 ni ahadi ya Katibu Mkuu mstaafu Abdulrahiman Kinana aliyoitoa Juni 21, 2015 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Katwe.
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema,Denis Luhende jana akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli baada ya hafla ya makabidhiano ya saruji mifuko 26 ya saruji ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya tawi la Katwe.Saruji hiyo ilitolewa na Dk. Bashiru Ally.
.Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na wananchi na wana CCM wa Kijiji cha Katwe (hawapo pichani) jana baada ya kuwakabidhi ifuko 26 ya saruji ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Chama ya tawi la Katwe.

Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM tawi la Katwe wakiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, wa nne kutoka kushoto mbele ya jengo la tawi hilo.Wa tano kutoka kulia ni Mwenyekiti wa tawi hilo, Ruben Mchembe.

……………………………………………

NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Katwe wilayani Sengerema, wamesema uongozi wa Chama taifa umedhihirisha kuwa wa vitendo baada ya Dk. Bashiru Ally kutekeleza ahadi ya mtangulizi wake, Abdurahman Kinana.

Wamesema CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Dk. Bashiru, wameonyesha kwa vitendo badala ya maneno kutokana na kutekeleza ahadi nyingi zilizoahidiwa kwa wananchi na wana CCM iwe kwa Chama ama serikali.

“Tufikishie salama kwa Mwenyekiti Rais Magufuli tunaridhishwa na utendaji wake lakini pia Dk. Bashiru, ahadi hii ni ya muda mrefu na sasa ameitimiza na inaonyesha CCM na viongozi wake walivyo wa vitendo na si wa maneno.Tunamini jengo letu litakamilika,”alisema Mwenyekiti wa tawi la Katwe, Ruben Mchembe.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum, akikabidhi ahadi hiyo ya mifuko 26 ya saruji yenye thamani ya sh.507,000 jana alisema, Kinana (Katibu Mkuu mstaafu) Juni 21, 2015 aliahidi kuchangia sh. 500,000 za ujenzi wa ofisi ya tawi la Katwe wakati akiweka jiwe la msingi.

Alisema hadi anang’atuka hakuwa ametimiza ambapo Agosti Mosi, mwaka huu Dk. Bashiru akiwa ziarani Sengerema katika Jimbo la Buchosa aliahidi kutekeleza kwa asilimia 100 ahadi hiyo ya Kinana, baada ya viongozi wa tawi la Katwe kumueleza wakikumbushia ahadi hiyo ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chama.

“Nimekuja hapa kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo ambayo ni mifuko 26 ya saruji kwa maelekezo ya Katibu Mkuu ( Dk. Bashiru) ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza ili mkamilishe jengo hili.Ahadi hii imetekelezwa kwa asilimia 100,” alisema Kalli akiahidi kuwaletea rangi likamilika walipake na kuonekana la kisasa.

Aidha kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Denis Luhende alipongeza jitihada za wana CCM wa Katwe kujenga ofisi ya Chama na kwa jitihada walizozionyesha wakiungwa mkono na Dk. Bashiru, watawasogea na kulikamilisha jengo hilo.

Naye Katibu wa CCM Kata ya Katwe, Francis Mahuma, aliahidi kuwa watasaimamia kwa dhati ujenzi wa mradi huo na kwamba bado wana changamoto ya samani za ofisi na siyo rangi tu.

“Kwa niaba ya wananchi na wana CCM wa Katwe,tunaamini jengo letu kwa mchango huu sasa litakamilika na hivyo tufikishie salamu na shukurani zetu kwa Dk. Bashiru kuwa alichotoa tumekipokea,”alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...