Na Leandra Gabriel,  Michuzi TV

JUKWAA la uziduaji lililoandaliwa na Taasisi ya Haki Rasilimali kwa mwaka 2019 limefanyika Jijini Dodoma na kutoka na mapendekezo mbalimbali ikiwemo ufaidi wa rasilimali kwa wananchi pamoja na matumizi sahihi ya mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji inayojumuisha rasilimali za mafuta  madini na gesi asilia pamoja na kuwashiriki sha wanawake katika sekta hiyo.

Kupitia jukwaa hilo lililowakutanisha wadau kutoka kote nchini mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo duru ya kisiasa na uzalendo wa rasilimali, ushirikishwaji wazawa na ufaidi wa wananchi kwenye sekta ya uziduaji, pamoja na mapato na matumizi yatokanayo na sekta ya uziduaji, ambapo masuala makubwa yaliyotawala ni pamoja na kutowaminya wanawake kuwashiriki katika sekta ya uziduaji aidha kwa imani potofu au vinginevyo.

Pia washiriki wameishauri Serikali kutunga sheria bila kuweka vikwazo ambavyo vitawaumiza wananchi wa chini na hiyo ni pamoja na wabunge kutopitisha  sheria kwa hati ya dharura kwa manufaa ya wote hasa wananchi wa kupata cha chini.

Vilevile washiriki wametoka na kauli moja ya kushirikiana, kuaminiana na kuhabarishana baina ya Serikali na azaki za kiraia kwa kujenga ubia katika kuhakikisha sekta ya uziduaji inaleta tija zaidi.

Kupitia jukwaa hilo washiriki waliotoka katika Mikoa yenye Rasilimali za madini ikiwemo Geita na Shinyanga wamezishauri kampuni zinazofanya shughuli za uziduaji katika maeneo hayo kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa wamiliki wa rasilimali hizo (wananchi) ikiwemo kujenga miundomiu ya shule, hospitali na miundombinu ya maji.

Pia kupitia jukwaa hilo washiriki wameishauri Serikali kwa kushirikiana na Azaki mbalimbali kuelekeza makampuni yaliyowekeza kwenye sekta ya uziduaji nchini kuto nafasi za ajira kwa wazawa na hiyo ni pamoja na kutoa nafasi za kusambaza huduma na  bidhaa katika maeneo ya kisekta.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na taasisi ya Haki Rasilimali lilitanguliwa na wiki ya Azaki ambapo viongozi  na wadau mbalimbali wa sekta ya uziduaji walitoa maoni ya kujenga na kuboresha sekta hiyo.

 Mkurugenzi mtendaji wa Haki Rasilimali  Racheal Chagonja akichangia mada wakati wa jukwaa la uziduaji lililofanyika jijini Dodoma,  Chagonja  amesema kuwa wataendelea kuhabarisha wadau kuhusiana na fursa zitokanazo na sekta ya uziduaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki Rasilimali Racheal Chagonja (kulia) wakionesha kitabu maalumu cha sekta ya uziduaji kilichozinduliwa na taasisi hiyo wakati wa jukwaa la uziduaji lililofanyika jijini Dodoma.
 Balozi  wa Canada nchini Pamel O'Donnell's (katikati) akichangia mada kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika sekta ya uziduaji ambapo ameeleza kuwa nafasi ya wanawake katika sekta hiyo ni muhimu, leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...