BAADA ya kutokea tafsiri na uelewa tofauti kuhusiana na wagombea wanaopaswa kushiriki uchaguzi mkuu wa Novemba 24 mwaka huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa ufafanuzi kuwa watakaowania nafasi za uongozi ni wale walioteuliwa au rufaa zao kukubaliwa.

Jafo ametoa ufafanuzi huo leo jijini Dodoma alipokua akizungumza na wandishi baada ya kuwapo kwa tafsiri nyingi zinazotofautiana kwa wadau mbalimbali wa uchaguzi.

Amesema Ili kuondoa tofauti ya uelewa ambao mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka 2019, ufafanuzi watakaowania uongozi huo ni wale wenye sifa.

Jafo ameongeza kuwa watakaoshiriki uchaguzi ni waombaji wote ambao walichukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za uongozi na kisha wakateuliwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.

Jafo amesema waombaji wote waliowasilisha pingamizi kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuomba kuteuliwa na pingamizi zao zilikakubaliwa
Jafo alisema pia ni wale waombaji wote waliokata rufaa kwenye Kamati za Rufaa za Wilaya na rufaa zao kukubaliwa.

“ Hivyo, ninawaelekeza wasimamizi wa uchaguzi katika halmashauri zote nchini kusimamia utekelezaji wa maelekezo haya kikamilifu,” Amesema Mh Jafo.
Waziri Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...