Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPENI ya "Linda Ardhi ya Mwanamke"  inayotekelezwa na asasi 26 za kiraia ambazo zinajihusisha na masuala ya ardhi kote nchini, kesho Novemba 21 zitazindua rasmi kampeni  hiyo huku mgeni rasmi wa hafla hiyo akitegemewa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kampeni hiyo Tike Mwambipile amesema; Tanzania imekuwa nchi ya Kwanza kuendesha kampeni hiyo katika ngazi ya kimataifa na kuwezeshwa na mashirika ya LANDESA ulimwenguni, Habitat for Humanity, Huairou Commission, Benki ya dunia pamoja na asasi za kiraia ambazo zitafanya tafiti za kina zinazolenga kuleta mabadiliko ya umiliki wa Ardhi baina ya wanawake na wanaume.

Amesema kuwa kuchaguliwa kwa Tanzania kuendesha kampeni hiyo ni kutokana na sheria nzuri za masuala ya Sheria licha ya kuwa na changamoto chache za utekelezaji.

Time amesema kuwa malengo ya kampeni hiyo ni kufunga umbwe lililopo kati ya sera, sheria na taratibu za maisha ya kila siku ya wanajamii ikiwemo kubadilisha fikra za wanajamii kutoka katika mila kandamizi zinazozuia wanawake kumiliki ardhi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi (LANDESA) na mratibu wa kampeni hiyo Monica Mhoja amesema kuwa kampeni hiyo imejikita katika mambo makuu manne ikiwemo kuondoa mila na desturi potofu zinazowakwamisha wanawake kupata haki zao katika ardhi pamoja na kuwawezesha wanawake kutumia ardhi zao kwa manufaa ya kiuchumi.

Vilevile amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wamejizatiti kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi na hilo ni pamoja na haki za wanawake za umiliki wa ardhi.

Amesema kuwa kampeni hiyo imedhamiria kuwawezesha wanawake kumiliki na kufaidi mapato yatokanayo na ardhi.

"Kuna baadhi ya maeneo wanawake huona ni kawaida kutoshirikishwa katika suala zima za umiliki wa ardhi na hiyo hutokana na kutokuwa na uelewa kuhusiana na usawa wa jinsia katika umiliki wa ardhi" ameeleza.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wanaamini kuwa wanawake wengi watapata maarifa ya kuelewa haki zao katika umiliki wa ardhi na haki za upatikanaji wa ardhi.

Asasi 26 za kiraia zitakazoshiriki katika kampeni hizo ni pamoja na TAMWA, SHIVYAWATA, LANDESA, TGNP mtandao na TALA.
Mratibu wa Kampeni ya Linda Ardhi ya Mwanamke Monica Mhoja (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kampeni hiyo ambayo imelenga kuwakomboa wanawake kuhusiana na suala zima la umiliki wa ardhi, kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo Time Mwambipile na anayefuatia ni Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...