Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi
mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao New
Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee
cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mama magufuli, ambaye aliambatana na Mlezi wa umoja huo Mke wa Waziri
Mkuu Mama Mary Magufuli, Mwenyekiti wake Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu
Mama Tunu Pinda na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa
misaada mbali mbali ya ujenzi, chakula na nguo.
Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais Mhe
Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya
ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Novemba
15, 2019 kilikuwa na wazee 26.
Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa
kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 1.9, vyakula na nguo
vyenye thamani ya shilingi milioni 3.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na wajumbe wa umoja wa wake
wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group akiwasili
katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam
leo. Wengine toka kushoto ni Mama Tunu Pinda, Mama Mary Majaliwa, Mama
Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako na Mama Asina Kawawa.
Wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New
Millenium Women’s Group wakiwa katika kituo cha kulea wazee cha Nunge
Kigamboni jijini Dar es salaam leo walikofika kutoa misaada mbalimbali
katika kuadhimisha umoja huo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada ya nguo na
vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es
salaam leo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akitoa misaada ya nguo na
vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es
salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na
wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New
Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha
kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na
wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New
Millenium Women’s na wakaaazi wa kituo cha kulea wazee cha Nunge
Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na wajumbe wenzie wa
umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s
baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha
Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...