TANZANIA kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya uwezeshaji mifugo ya maziwa ya Land o'Lakes imezindua mradi wa miaka mitano wa uzalishaji bora maziwa na kuongeza soko la bidhaa za maziwa nchini ifikapo mwaka 2024.

Akizindua mradi huo jijini Dar es salaam leo Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huo unazingatia uwezeshaji kwa maafisa ugani mikoa 26 ya Tanzania bara na kwamba utaanza kutekelezwa katika mikoa minne ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huo utazingatia kuwezesha maafisa ugani, pembejeo na uzalishaji wenye tija hadi kufikia mahitaji ya soko la bidhaa za maziwa ndani na nje ya nchi.

Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huu ambao unaungwa mkono na inchi kadhaa za wahisani ikiwemo Marekani unalenga pia kuunga mkono juhudi za rais wa awamu ya tano Mhe. Dk John Pombe Magufuli katika kuhakikisha inchi inakuwa katika uchumi wa viwanda na kujitegemea kiuchumi.

Amesema kwa sasa Tanzania bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa licha ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo huku  sekta ya Mifugo ikiabiliwa na changamoto za ugani, anautaja mradi huu kuja na ufumbuzi wa kuhakikisha uzalishaji maziwa unaongezeka mara dufu.

Hata hivyo  Prof. Elisante Ole Gabriel  anawataka watanzania kupokea mradi huu kwa mikono miwili na kuondokana na ufugaji wa kuchunga kuelekea ufugaji wa kibiashara na kuiwesha nchi kuongezea thamani bidhaa za maziwa kwa mahitaji ya ndani na nje ya nchi

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu Tanzania inayo mifugo Ngombe Milioni 30 Mbuzi Milioni 20.5 Kondoo Million 5.5 lakini wanaotumika katika uzalishaji maziwa ni Milioni mbili tu.

Kwa upande wa mratibu wa mradi huo nchini Tanzania kutoka taasisi ya LAND O’LAKES Bi. Neema Mrema amesema mradi huo  pia unatekelezwa katika nchi kadhaa barani  Afrika ambapo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuinua pato la wafugaji na nchi husika kwa ujumla.

Amesema taasisi hiyo ya kimataifa imekuwa ikitekeleza miradi hiyo kwa kuwawezesha maafisa ugani na pembejeo za kisasa kwa manufaa ya kuleta tija ya ongezeko la uzalishaji wa maziwa kutoka Ng”ombe mmoja kukamuliwa lita 5 hadi 15 kwa siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...