Na Said Mwishehe, 
Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amewataka wakulima wote nchini kuuza mazao yao kwa bei wanayotaka na kwamba Serikali haitapanga bei na badala yake jukumu hilo libaki kwa mkulima mwenyewe.

Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Novemba 20, mwaka 2019 akiwa katika eneo la Dumila mkoani Morogoro.Rais alisimama kuzungumza na wananchi hao akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma kikazi.

Akiwa na wananchi hao, Rais Magufuli amekumbusha kuwa mvua zimeanza kunyesha, hivyo watu wajihusishe na kilimo huku akieleza kuwa kuna watu wanalalamika kupanda kwa bei ya mahindi lakini ifahamike Serikali haitapanga bei.

Amesema mkulima mwenyewe ndio ataamua anataka kuuza bei gani kulingana na mahitaji ya soko kwa wakati husika.

"Nataka Mkoa wa Morogoro uwe kinara katika kuzalisha mazao.Serikali ninayoingoza katika kipindi changu sitapanga bei ya vyakula, wakati mkulima analima hakuna anayempangia bei, hivyo anapouza mazao yaake aachwe aamue anataka kuuza bei gani mazao yake,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza hata kama mkulima ataamua kuuza debe moja la mahindi kwa Sh.milioni moja sawa tu auze. "Hakuna kumpangia bei, wanaotaka bei nafuu wakalime wao."

Amefafanua ni kama ilivyo kwa mfugaji, anapouza ng'ombe huangalia bei ya soko , kama bei ya ng'ombe itakuwa juu atauza kwa bei ya juu, hivyo wakulima nao waachwe wapange bei wenyewe."Soko liachwe liamue bei na sio kupangiwa na Serikali."

Amesisitiza watu waache kulalamika mahindi yamekuwa juu na hiki ndio kipindi cha wakulima kunufaika na kilimo chao."Hata anayekuwa ofisini bado anaweza kulima kwa kutumia fedha zake kumtuma mtu amlimie badala ya kulalamika tu."

Rais Magufuli amesema kwa sasa soko la mahindi na mazao mengine ni nzuri na kuongeza nchi nyingi zinahitaji kununua mazao kutoka kwa wakulima wa Tanzania, hivyo ni wakati wao kutajirika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...