Mwonekano wa Jengo la katika jengo la MNF  ambamo kuna hoteli ya Johari Rotana

 Baadhi ya picha za vitu na samani zinazopatikana katika hoteli ya yota tano Johari Rotana inapatikana katika jengo la MNF katikati ya jiji la Dar es Salaam ikiwa na vyumba vikubwa 253, vyumba vya kifahari na makazi.
Baadhi ya Misosi inayopatikana katika Hoteli Mpya ya Johari Rotana.


KATIKA jitihada za kuongeza uwepo wake katika sekta ya utalii inayokuwa kwa kasi barani Afrika, Rotana ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika uendeshaji wa hoteli barani Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya na Uturuki, imetangaza leo ufunguzi rasmi wa hoteli ya hadhi ya nyota tano ya Johari Rotana ndani ya jiji la Dar es Salaam. Hoteli hiyo ndiyo imefungua mlango kwa kampuni hiyo katika soko la Afrika Mashariki.

Hoteli hiyo yenye mandhari ya kuvutia inapatikana kwa urahisi kabisa ndani ya jengo la MNF lililopo katikati ya jiji. Pamoja na kuwa na vyumba vya kukodi vipatavyo 60 vyenye samani ndani yake, Johari Rotana ina vyumba 253 vyenye ukubwa wa kutosha ikiwemo vyumba 193 vya kifahari. Kupitia vyumba vya hoteli hiyo vilivyopo kuanzia ghorofa ya 13 kwenda juu, mkaaji anaweza kuona na kufurahia mandhari ya kuvutia ya bandari na jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia ufunguzi huo, Guy Hutchinson, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Rotana alisema: "Kama sehemu ya mkakati wetu wa muda mrefu, Afrika inaendelea kuwa soko muhimu sana
kwa Rotana. Kupitia ufunguzi wa hoteli hii ya Johari Rotana, kampuni yetu imetimiza hatua muhimu katika safari yetu. 


"Tumeweka viwango vipya katika usanifu majengo, muundo, teknolojia, na ubora wa huduma. Tunategemea hoteli hii ya Johari Rotana ambayo ni ya kwanza kwetu katika kanda ya Afrika Mashariki italeta ladha ya kipekee katika sekta. Tuna uhakika kwamba kuwepo kwa huduma mbali mbali za kukidhi mahitaji ya wateja ikiwemo vyumba vyenye ukubwa wa kutosha, vyakula na vinywaji vya aina mbalimbali, huduma za kisasa za mikutano ikiwa ni pamoja na kuwa na ukumbi mkubwa zaidi nchini wa kufanyia mikutano na sherehe – tumejiweka katika nafasi nzuri sana ya ushindani katika soko".


Hata hivyo Mwenyekiti wa kampuni miliki CRJE Ltd (Afrika Mashariki) Hu Bo, alisema: "Tuna miaka 50 ya utendaji bora nchini Tanzania, na tunafurahi sana kufungua hoteli hii ya kisasa zaidi ya Johari Rotana. Tunajivunia kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu katika sekta hii na kutangaza vivutio maarufu vya watalii vya nchini ikiwemo jiji la biashara la Dar es salaam.

"Johari Rotana ni hoteli ya tisa ya kiwango cha nyota 5 ambayo tumejenga nchini Tanzania. Kwa uzoefu wetu mkubwa katika biashara ya ujenzi wa hoteli na katika soko hili linalobadilika, tunaelewa vizuri mahitaji ya wateja, na kwa hakika Johari Rotana itakidhi mahitaji haya".

"Ningependa kuwashukuru washirika wetu kutoka bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), kitengo cha uwekezaji cha Benki ya Dunia, kama mashirika makuu katika mradi huu, pamoja na kampuni ya Rotana, ambayo tumeshirikiana nayo kusimamia jengo hili. Tuna uhakika kuwa hoteli yetu mpya itakidhi mahitaji ya soko yanayokua na itatoa huduma ya kipekee kwa wageni na wakazi wa jijini Dar es salaam".

Johari Rotana ina migahawa minne maridadi itakayo toa huduma ya vyakula vya aina tofauti ikiwemo Kibo Lobby Lounge, mgahawa wa siku nzima wa Zafarani, mgahawa wenye vyakula asili vya Kichina Noble House na mgahawa uliochangamka na wenye burudani wa Hamilton Gastropub.

Vivutio vingine vya hoteli hii ni pamoja na ukumbi mkubwa wa mikutano nchini Tanzania, bwalo la hoteli kubwa zaidi Tanzania lenye ukubwa wa mita za miraba 900 na paa lenye urefu wa mita 6.5 ambalo pia linaweza kugawanywa katika kumbi ndogo tatu. Hoteli hii pia ina kumbi zingine
sita za mikutano, kituo cha huduma za biashara, ofisi zenye hadhi ya juu, na eneo la maegesho ya magari kwa ndani, na hivyo kuifanya hoteli hii kuwa ni sehemu hakika kwa wageni wa kibiashara na mapumziko.

Wageni wanaokaa Johari Rotana pia watapata fursa ya kuchagua huduma mbali mbali za mazoezi na tiba za mwili, pamoja na bwawa la kuogelea la nje, vifaa vya mazoezi ikiwemo ulingo wa ndondi, na huduma nyingine mbalimbali za kiustawi wa mwili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...