Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

UKAGUZI  unaofanywa katika mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mererani Kaskazini mwa Tanzania, umeelezwa unawadhalilisha wanawake kwa kile kinachodaiwa wanawake huvuliwa nguo na kuachwa utupu mbele ya watoto wadogo hata wakionesha ushirikiano katika zoezi la ukaguzi.

Akizungumza jana jijini Dodoma katika Jukwaa la tisa la sekta ya AZAKI inayoendelea jijini Dodoma, Kanaeli Minja ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini hayo kutoka jijini Arusha ameeleza kuwa licha ya Serikali kutoa mwongozo wa kufungwa kwa mashine za ukaguzi,lakini  hadi  sasa mashine hizo hazijafungwa na wameendelea kudhalilika kwa kuachwa utupu hata wakionesha ushirikiano katika zoezi hilo la ukaguzi.

Kanaeli ameiomba Serikali kukemea tabia hiyo pamoja sambamba na viongozi wanaosimamia mgodi huo kufunga mashine hizo ambazo zitarahisisha ukaguzi na kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Aidha ameishauri Serikali kutunga sheria kwa kuangalia wananchi wa chini na wabunge wasipitishe sheria kwa hati ya dharura kwa kuwa wananchi wa chini ndio wanaoathirika zaidi.

Wiki ya AZAKI imezinduliwa hivi karibuni  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa jijini Dodoma.

Akifafanua shutuma hizo Naibu Waziri wa Madini Mh,Stanslaus Nyongo, amesema kuwa sio kweli kuwa watu wananyanyaswa ispokuwa wengi wao hawataki kutoa ushirikiano wakati wa Ukaguzi,amesema kuwa skana zinanzotumika kukagua madini hayo ni maalum na ni za ghalama kubwa. 

‘’Si kweli kwamba watu Wananyanyaswa,baadhi yao hawataki kutoa ushirikiano wakati wa Ukaguzi,ndio maana Maofisa wetu inabidi wawabane,kuhakikisha hakuna anaetoroka na madini hayo kwa namna yoyote ile’’,amesema Mh.Nyongo. 

Amesema mashine zinazotumika kukagua madini hayo ni ghali sana na teknolojia yake ni kubwa,lakini  wameisha iagiza inakuja,hivyo changamoto zote hizo zitaondoka,kwa hiyo inawezekana hayo mambo yanatokea lakini kwa wale ambao hawataki kutoa ushirikiano wakati wa ukaguzi. 

“Mtu asipotoa ushirikianao wakati wa ukaguzi inabidi maofisa wetu wawababane,kuhakikisha hakuna anaetorosha madini hayo, kwa sababu ni madogo sana,lakini pia nasisitiza Kwakweli hatutaki akinamama wadhalilishwe,kwa sababu Nchi yetu inapinga unyanyasaji wa kijinisia na Maofisa wetu wasimvue nguo mtutu yoyote ambaye ametoa ushrikiano”,alisema Nyongo.
Kanaeli Minja  mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite kutoka jijini Arusha 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...