Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC SACCOS) kimepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ambapo akiba za chama zimeongezeka kufikia Shilingi 97,933,820.00 kutoka Shilingi 39,827,800.00  mwaka 2017 kilipoanzishwa rasmi, sawa na ongezeko la Shilingi 58,106,020.00.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa chama hicho, Aron Ibrahim amesema Hisa za lazima zimefikia Shilingi 25,765,000.00 na chama kimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi 153,850,000.00.

Aidha, katika kipindi hicho, jumla ya kiasi cha Shilingi 114,118,411.00 kimesharejeshwa chamani na faida ya shilingi 16,779,250.00 imepatikana. Vile vile, jumla ya mikopo iliyopo kwa wanachama ni shilingi 137,283,945.00 hadi Oktoba 2019.

Katika mkutano huo Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCDC SACCOS walipokea Taarifa ya Kamati ya Usimamizi kwa kipindi cha mwezi Januari 2019 hadi Septemba 2019 iliyosomwa na mwenyekiti wa Kamati, Boniphace Moshi ambapo alisema hali halisi ya hisa na mtaji wa chama kwa pamoja umefikia  Shilingi 119,466,070.00.

Vilevile Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCDC SACCOS walipokea Taarifa Huru ya Mkaguzi wa nje ya mwaka wa fedha ulioishia 2018 kwa Wanachama kuhusu Taarifa ya Wakaguzi na Taarifa ya za TCDC SACCOS kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 31 Desemba, 2018. Taarifa hiyo ya ukaguzi uliofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ilionyesha kuwa chama kwa mwaka 2018 kimepata Hati yenye Mashaka.

Mkaguzi Dorah Meta  kutoka COASCO amesema baadhi ya mapungufu yaliyobainika mwaka uliotangulia yamefanyiwa kazi na amewapongeza viongozi wa TCDC kwa kuhakikisha kuwa dosari zilizobainika wakati wa ukaguzi uliotangulia zimeondolewa.

Katika mkutano huo, viongozi wapya wa TCDC SACCOS walichaguliwa baada ya waliokuwepo kumaliza kipindi chao cha miaka mitatu (3). Waliochaguliwa ni Aron Ibrahim aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti,  wajumbe wapya wa Bodi waliochaguliwa ni Boniphace Moshi, Ndinagwe Mwambola, Petronila Shirima, Ally Ndenya, Biyaga Nzohumba na Baraka Lukio; na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi ni Jackson Mushumba, Josephat Simkoko na Consolata Kiluma.
Mwenyekiti wa TCDC SACCOS, Aron Ibrahim akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Makamu Mwenyekiti wa TCDC SACCOS, Boniphace Moshi akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu  wa TCDC SACCOS wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Viongozi wapya wa TCDC SACCOS waliochaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...