WAKAZI wa Mkoa  Singida na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 18 lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.

 Mkuu wa Kanda ya Kati  wa TCRA  Anthony Manyanda amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa Singida kufika Stendi ya zamani ya mabasi kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa  kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Manyanda amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano..

Manyanda  amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ni huu na kuacha kusubiri mwisho wa mwezi Desemba.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Manyanda amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata ili waweze kusajili laini za simu kwa kwa  alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo lilipotolewa.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema.Manyanda.

Manyanda amesema kuwa Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika kanda ya Kati.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa elimu ya usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole ikiwa ni Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.
 Wananchi wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kuangalia namba ya vitambulisho katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.


 Matukio mbalimbali katika picha katika usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.
 Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Anthony Manyanda akizungumza na Wananchi wakati wa utoaji wa elimu ya usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole wakati wa Kampeni ya Mnada Kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.
Mwananchi akisoma fomu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA ili kuweza kukamilisha usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole,Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...