WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akijibu mwaswali ya Wabunge leo Novemba 14.2019 katika kipindi cha maswali ya Papo kwa papo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) na mbunge wa Viti Maalum, Oliver Semguruka Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 14.2019.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

…………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usambazaji wa huduma ya nishati ya umeme linaloendelea kufanyika nchini hususan kwenye maeneo ya vijiji kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni endelevu.

”Mheshimiwa Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme ifikapo 2021. Kazi hiyo inaendelea vizuri kwa usimamizi wa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 14, 2019) katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza.

Mbunge huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu vijiji ambavyo bado vitakuwa havijaunganishiwa umeme hadi 2021 ambao ni muda wa ukomo wa miradi ya REA.

Waziri Mkuu amesema hakuna kijiji kitakachokosa kuunganishiwa huduma hiyo na ili kuhakikisha inawafikia wananchi wote gharama za kuunganisha umeme vijijini zimepunguzwa na sasa ni sh 27,000 tu.

Amesema mbali na kupunguzwa kwa gharama za kuunganishiwa umeme, pia Serikali imefuta gharama za bidhaa nyingine za kupeleka umeme kwenye maeneo yao ikiwemo nguzo na nyaya.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kwenye sekta za afya, elimu na kilimo na hivi sasa inatarajia kutoa vibali 16, 000 vya ajira za walimu na kisha itatoa vya watumishi wa afya.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, ambaye alihoji, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wanapatikana watumishi wa kutosha kuwahudumia Watanzania.

Amesema mkakati wa kujenga miundombinu ya kutolea huduma mbalimbali nchini unakwenda sambamba na kuajiri wataalamu watakao wahudumia wananchi katika maeneo husika.

”Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira katika sekta hizi mbili za afya na elimu, hata kwenye kilimo. Mwaka jana tuliajiri watumishi 6,000 na sasa tuna kibari ambacho kitatoka hivi karibuni cha watumishi 16,000 kwa upande wa sekondari na msingi.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...