Yatambulisha menyu mpya ya USSD kwa huduma binafsi 

‘Customer Service’ sasa kuitwa ‘VODACARE’ 

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania PLC, hivi karibuni iliadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, kwa kutangaza mabadiliko katika mfumo wake wa huduma kwa wateja. Lengo la mabadiliko hayo ni kutoa uhuru kwa wateja wake kupata huduma kwa urahisi pale inapotakiwa.

“Tuna zaidi ya njia nane ambazo mteja anaweza kuzitumia kutufikia na leo tunaiongeza nyingine ambayo itampa mteja fursa ya kujihudumia; hii ni menyu ya USSD, ambayo inapatikana katika simu,” alisema Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom, Harriet Lwakatare

Kwa kupiga *149*01# mteja anaweza kufanya miamala ya M-Pesa, kuangalia taarifa za matumizi, kupata huduma muhimu kama vile kununua Luku, kuangalia salio, kifurushi cha intaneti na taarifa kuhusu bidhaa mbalimbali za Vodacom. 

“Kwa idadi ya zaidi ya wateja milioni 14, kitengo cha huduma kwa wateja ni kati ya vitengo vyenye kazi muda wote. Vodacom inaendelea kukua kiteknolojia na kuwapa huduma ya kidigitali wateja wake ili kutoa huduma endelevu kupitia njia kadha wa kadha 

“Tunajali mahitaji ya wateja kwa huduma ya haraka na nyepesi. Ndio maana hatujachoka kufanya kazi na kuendelea kuwapa wateja wetu kilicho chaguo kwao na hasa linapokuja suala la kuhitaji msaada. Tuna huduma kwa wateja kwa njia ya kidigitali kupitia WhatsApp, Mitandao ya kijamii, majibizano kwa njia ya sauti (IVR) na mawasiliano ya moja kwa moja. Na sasa tunawaletea menyu ya USSD kwaajili ya huduma binafsi kwa mteja,” alisema Harriet.

Katika hatua nyingine, Harriet alisema kuwa, kuanzia sasa njia zote za huduma kwa mteja zitakuwa zikifahamika kama VODACARE; hii ni ishara kwa Vodacom kuwa imeamua huduma binafsi na za kipekee kwa wateja 

“Tumebadilisha jina la ‘Customer Care’ kwenda ‘VODACARE’ sambamba na maboresho ya kipekee tuliyoyafanya katika kitengo cha huduma kwa wateja ya kwa kiwango cha hali ya juu,” alisema Harriet

Huduma za VODACARE zinapatikana kwa mteja kupiga 100/01 kwenda kituo cha huduma au kwa kutumia mitandao ya kijamii; WhatsApp, mawasiliano ya moja kwa moja au My Vodacom App, menu ya msaada binafsi na katika maduka yote ya Vodashops na kupitia dawati la huduma.

“Aliongezea kusema “Wiki hii Vodacom si kwamba inasherehekea nguvu ya huduma bora kwa wateja kama sehemu ya maudhui yake, ila tunasema kwamba ukiwa na Vodacom matumizi na upatikanaji wa msaada wa huduma kwa mteja ni rahisi wakati wote kupitia katika njia zetu zote za mawasiliano,” alimalizia kusema Harriet

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...