Na Karama Kenyunko, Globu ya Jami.

WABUNGE  watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotaka wabunge wanne wa chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge waliokamatwa leo Novemba 18, 2019 ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa huku a Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye alishakamatwa wiki iliyopita

Heche na Msingwa wamekamatwa leo mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.

Wabunge hao wameunganishwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika kituo hicho cha Osterbay huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidaiwa kuwa anaumwa na amelazwa.

Novemba 15, mwaka huu 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru wabunge hao wanne wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kutokufika mahakamani hapo bila ya kutolewa taarifa yoyote wakati kesi yao ya uchocgezi ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Kesi hiyo inatarajia kuendelea Novemba 19, 2019 (Kesho) kwaa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizwaji.

Kabla ya kutoa amri hizo, Novemba 15, mwaka huu kesi  hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, ambapo washtakiwa wengine waliwahi lakini wabunge hao wanne hadi saa 4:05 asubuhi walikuwa hawajafika mahakamani bila sababu za msingi.

Washtakiwa waliofika mahakamani Novemba 15, 2019 ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

Katika Kesi hiyo Mbowe na wenzake wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.
Pia, wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam..


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...