Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Yespa Manispaa ya Morogoro wakiwa nje ya nyumba zilizozingirwa na maji.
……………………………..

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Baadhi ya kaya zilizo kandokando ya Mto Ngerengere Mtaa wa Yespa Manispaa ya Morogoro zimezingirwa na maji na kusababisha wakazi wa mtaa huu kuhama  kwa muda, ambapo imeelezwa hali hiyo imesababishwa na Maji kupoteza mwelekeo baada ya sehemu ya mto kuzibwa katika ujenzi wa Reli ya kisasa.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kuwa hali hiyo imesababishwa na maji kupoteza mwelekeo kufuatia ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa ambao imesababisha maji kujaa katika makazi ya watu.
Aidha wakazi hao wamesema kuwa  hali hiyo ya maji kuingia kwenye maeneo ya makazi imetajwa kusababisha hasara, ambapo licha ya baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao kwa muda, pia baadhi ya huduma zimesimama ikiwemo ibada.

Wakazi hawa walio pembezoni mwa mto Ngerengere wamesema kuwa wengi wao wameishi kwa muda mrefu katika maeneo hayo lakini  wajawahi kukutana na changamoto ya kuzingirwa na maji hivyo swala hilo kwao wanaliona ni tatizo hivyo wanaiomba mamlaka husika kulichulia hatua.
Pamoja na kaya zilizo zingirwa na maji kuwa pembezoni mwa mto Ngerengere, Malalamiko ya wakazi hao ni ujenzi wa Reli ya kisasa, wakidai sehemu kubwa ya mto imezibwa ambapo kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha mto huo umefurika na maji kusambaa baada ya kukosa mwelekeo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...