Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na washiriki wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiserikali
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na washiriki wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiserikali
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiagana na mtakimwi mkuu wa serikali Dr Albina Chuwa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiserikali

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Watafiti wote wanaofanya utafiti Tanzania wametakiwa kufanya utafiti wakiwa wanaelimu ya utafiti kutoka chuo cha takwimu hapa nchini au nje ya nchini kwa lengo la kuondoa takwimu zisizo sahihi ambazo zimekuwa zikileta migogoro kwenye jamii.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema kuwa watakwimu wote wanatakiwa kufanya tafiti wakiwa na cheti kinachomsibitisha kuwa ni mtakwimu.

“Wanaojiita mtakwimu yeyeto yule lazima awe na cheti ambacho kinamdhibitisha kuwa ni mtakwimu na amesaini maadili ya takwimu la sivyo atakuchuliwe hatua za kisheria na pia hataruhusia kufanya kazi za kitafiti katika eneo usiku” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa watakwimu wakitoa takwimu ambazo sio sahihi sinaleta tatizo kwenye usalama wa taifa kwa unakuwa umetikisa usalama wa taifa.

“Huyu mama na watu wake ni muhimu sana kwa usalama wa nchini kwa kuwa wanatoa takwimu zilifanyiwa kazi na zimethibitishwa na mamlaka husika” alisema Kasesela.Aidha Kasesela amesema kuwa watafiti wengi wanatakiwa kurudi darasani ili kuwasaidia kutoa takwimu zilizo sahihi na zisizoleta madhara kwa usama wa taifa.

Awali akitoa maelezo kwa ufupi kwa mgeni rasmi,mtakimwi mkuu wa serikali Dr Albina Chuwa amesema kuwa watatumia technolojia ya hali ya juu kukusanya takwimu zilizo sahihi kwa muda mfupi.

“utafiti huu kwa weledi wa juu wa kutumia teknolojia ya Kisasa ya kusanya takwimu Nchi nzima kwa muda mfupi na kupunguza gharama na Utafiti huu umgefanyika miaka kumi kumi iliyopita ungegharamiwa kwa Tshs. Bilioni 5 lakini kwa matumizi ya teknojia ya Tablets imepunguza gharama kwa nusu,Utafiti huu utagharimu TShs. Bilioni 2 na Matokeo yatatolewa mwezi Desemba 2019” alisema Chuwa

Hata hivyo Chuwa alisema dhahiri teknolojia kwa kiasi kikubwa imepunguza gharama za kufanya Tafiti hapa Nchini na nitumie nafasi kutoa wito kwa Watakwimu wote Nchini kuwa ni vyema tujikite zaidi katika kuendeleza kujifunza zaidi teknolojia za kisasa za kuchakata taarifa za Kitakwimu kwa kuwa kwa sasa Dunia kila siku mbinu mpya za kitakwimu zinaendelea kufanyiwa majaribio na kutumika na Maofisi ya Takwimu Duniani. 

“Napenda kuwaomba Benki ya Dunia na IMF kuendelea kuzijengea uwezo Ofisi za Takwimu za Afrika katika Matumizi ya teknojia mbali mbali za kuchakata takwimu wakati tunapoelekea kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2030” alisema Chuwa

Aidha Chuwa alisema kuwa hanashaka na matokeo ya Utafiti huu kwa kuwa juhudi zinazoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mpendwa wetu Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na uchumi wa Viwanda asilimia za upatikanaji wa yakavuka malengo yaliyowekwa katika Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme hapa Nchini. Miradi ya Kimkakati iliyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Maendeleo -2016/ 17 2020/21 umebainisha mikakati ya upatikanaji wa umeme wa kutosha hapa Nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...