Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urioh.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya kubadili Tabia na Uongozi yaliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari ya Connerstone iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha.
Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakishangilia baada ya mwenzao kuonyesha kipaji chake (hayupo pichani)

Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakifuatilia kwa makini kile kilichokuwa kinaendelea katika Mafunzo hayo.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, jamii imetakiwa kuwajengea uwezo Watoto ,kuziishi ndoto zao na kutambua kuwa Watoto huanza Maisha pale wanapozaliwa ,hivyo kila hatua iwe wezeshi kwa watoto kufikia ndoto zao.

Limekuwa ni jambo la kawaida katika jamii kubwa za kiafrika ,wazazi au walezi kuwalazimisha Watoto wao kufikia ndoto ambazo wao hawajazifikia, na haswa kwa kutumia mifumo rasmi kama ya Elimu ambayo inamuandaa mtoto kuwa kama jamii inavyotaka na siyo kama apendavyo yeye mwenyewe

'’Utamsikia mzazi akimlazimisha mtoto wake kwa kumwambia nataka usome uje kuwa daktari,askaripolisi,Mwanajeshi,mwanasheria,mwalimu,bila kumsikiliza mtoto anapenda kuja kuwa nani ili aweze kumtilia mkazo Zaidi katika jambo lile alipendalo’’

Daniel Urioh ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika amewaambia waandishi wa habari kuwa wazazi wawe na muda wa kukaa na watoto wao, wapate kuwasoma, kujua vitu wanavyoelekea kuvipenda waanze kutilia mkazo ,ili waweze kuwakutanisha na watu ambao wamefanikiwa katika sekta hizo, ili kuwajengea hamasa za kufikia ndoto zao.

''Mazingira ya mtoto huanzia nyumbani pamoja na wale wanaomzunguka,mifumo sikivu kwa ndoto za watoto siyo kuwafanya waishi kwa matakwa ya kile wanachokipenda wazazi , jambo ambalo linapelekea mtoto kukwama kufikia malengo yake pindi anapokuwa mtu mzima na kuanza kujitegemea’’alisema Mkurugenzi 

Ametoa wito kwa walimu ambao wananafasi kubwa katika Maisha ya Watoto,kwa kuwa nao muda mwingi zaidi katika mazingira yao haswa shuleni kuliko mtu mwingine yeyote, watumie nafasi hiyo kulea ndoto, vipaji, ubunifu wawatoto hao kwa mbinu zisizodhalilisha,kuumiza au kuwakatisha tamaa (non-violence strategies)

‘’Baadhi ya walimu wamekuwa na tabia ya kuua ndoto, vipaji na ubunifu wa Watoto kwa lugha za kidhalilishaji,za kuumiza na kukatisha tamaa Watoto jambo ambalo siyo zuri kabisa’’alisema Daniel.

Aidha katika kuadhimisha siku ya Watoto duniani Elimu ya Afrika inachukua jukumu la kuleta suluhu kwa kutumia programu na makongamano ya kuwatia moyo, kuwatengenezea majukwaa ya kujifunza na kuonyesha vipaji na bunifu zao.

Amesema kuwa Vijana hupata nafasi kushirikiana kwa pamoja, kuhamasishana kuleta majibu ya changamoto zinazowazunguka na mwisho hutumia vipaji kuburudisha pia.

Siku ya watoto duniani huadhimishwa kila mwaka duniani ambapo ilianzishwa na mwaka 1954 na husheherekewa tarehe 20 mwezi wa novemba kila mwaka kwaajili ya kuhamasisha na kueneza uelewa miongoni mwa Watoto duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...