Charles James, Michuzi TV

WAZIRI MKUU Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa Afya wa kidijitali utakaofanyika Novemba 14 mwaka huu jijini Dodoma.

Mkakati huo wenye lengo la kufanya maboresho kwenye sekta ya Afya umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais-TAMISEM ambapo unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa mojawapo ya wa Nchi viongozi ulimwenguni katika afya ya kidijitali.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mkurugenzi Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe amesema mojawapo ya mambo muhimu kwenye mkakati huo ni muundo wa utawala ambao unaongeza meno na ufanisi katika mkakati tekelezaji wa mkakati huo.

" Viungo viwili vikuu vitawajibika kimsingi katika mkakati huu navyo ni Kamati ya usimamizi wa afya ya kidijitali na Sekretarieti ya Afya ya Kidijitaki Kitaifa," Amesema Dk Grace.

Amesema mkakati huu mpya wa kitaifa ni wa miaka mitano hadi 2024 na utaenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2024, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (2015-2020) na sera zingine muhimu zinazohimiza juhudi Nchi kujenga mifumo madhubuti ya kidijitali inayoweza kuwasiliana na sekta ya afya.

Vilevile amesema Serikali inatarajia kuzindua maktaba ya kidijitali kuhakikisha kuwa kuna uwazi na wadau wanapata taarifa juu ya mipango iliyopo ya afya na hati zote.

" Sambamba na wiki hii kutarajia kuzindua mpango huu kuna Kazi nyingi ambazo zinaendelea kwenye viwanja vya Jamhuri ikiwemo kupika afya ya magonjwa yasiyoambukiza na tunashukuru mwamko wa wananchi umekua mkubwa ingawa tunasisitiza waziri kujitokeza kwani hakuna malipo yoyote.

Pia tutazindua mpango wa magonjwa yasiyoambukiza ambapo moja ya Kazi ya mkakati huu wa kidijitali ambao pia tutauzindua itakua kuhifadhi takwimu za magonjwa yasiyoambukiza, lazima tuweze kufuatilia rasilimali zote zinazoingia kwenye huo mpango je zinaleta tija? Lakini pia tuwe na taarifa muhimu za haya magonjwa je zinaongezeka au zinapungua," Amesema Dk Grace.

Amesema wao kama Wizara wameamua kwenda na mpango huo wa kidijitali ili kuwa na Benki ya takwimu lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa sekta ya afya nchini.Mpango huo unatajwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 na umeandaliwa kwa muda wa miezi sita hadi kukamilika.

Dk Grace amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kupima afya zao sambamba na kufanya mazoezi ambayo yamekua muarobaini wa magonjwa yasiyoambukiza." Sekta ya afya ni sekta ambayo inabadilika sana, kila siku magonjwa mapya na tiba mpya zinakuja, mpango huu utakua msaada kwenu tutakapohitaji kufanya tafiti maana tutakua na takwimu ya kile tunachohitaji kukifanyia utafiti.

Sasa mfumo huu wa kidijitali utatusaidia sasa kuangalia zile takwimu zetu na kuzifuatilia kuona kama kuna mambo mapya yanatokea ni kwanini kwahiyo tutatumia takwimu zetu kufanya tafiti. Mpango huu wa kidijitali unaenda kuwa mkombozi kwenye sekta hii muhimu ya Afya," Amesema Dk Grace.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Grace Mapunda akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa afya ya kidijitali utakaofanyika Novemba 14 mwaka huu jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...