Gari likiwa limebeba ng’ombe waliotolewa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim kwa waumini wa Kiislamu pamoja na BAKWATA,kwa ajili ya kitoweo cha maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela,wa tatu kutoka kushoto akitoa neno wakati wa kukabidhi ng’ombe watano wa kitoweo waliotolewa kwa BAKWATA mkoani hapa kwa ajili ya sherehe za maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W yanayofanyika kitaifa Mwanza, Novemba 9.

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hassani Kabeke, wa kwanza kushoto akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa, John Mongela (wa pili kutoka kushoto) baada ya kumkabidi saruji mifuko 100 iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kwa ajili ya ujenzi wa msikiri wa BAKWATA mkoani humu jana. Picha zote na Baltazar Mashaka





Kaimu sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, alhaji Hassani Kabeke akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kukabidhi kitoweo kwa waumini wa dini hiyo kwa ajili ya maulidi lakini pia saruji ya ujenzi wa msikiti jijini humu.
.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Furahisha Kirumba, Manispaa ya Ilemela kabla ya kuwakabidhi ng’ombe watano wa kitoweo waliotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim lakini pia mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Bakwata mkoani huu jana.
…………………………………………………….

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Kassim ametoa ng’ombe watano kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya sherehe za Maulidi.

Ng’ombe hao wa kitoweo walikabidhiwa juzi kwa kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke na Mkuu wa Mkoa huo John Mongela kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Akizunguza wakati akikabidhi ng’ombe hao kwenyeViwanja vya Furahisha, Kata ya Kirumba katika Manispaa ya Ilemela zinakofanyikasherehe hizo kitaifa, Waziri Mkuualisema kitoweo hicho kitawasaidia Waislamu katika kipindi hiki cha kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W.

Waziri Mkuu aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu wanaposherehekea maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume wahakikishe wanadumisha mshikamano,amani na utulivu wa nchi, tunu pekee inayoliliwa na mataifa mengi duniani.

“Niwatakie sherehe na maadhimisho mema ya maulidilakini jambo pekee na muhimu tuhakikishe tunafanya kwa utulivu, amani na mshikamano,ingawajambo hili kubwa ni kuwajenga watu kirohona kiimani,”alisema.

Sheikhe Kabeke akizungumza baada ya kupokea kitoweohicho kwa niaba ya BAKWATA na waislamu, alisema kitoweo hicho ni kafara njemaisiyo na doa.

“Serikali haina dini, ni faraja kwetu sisiWaislamu kutuunga mkono kwa kitoweo hiki ambacho ni kafara kubwa.Hii ndiyoserikali tunayoitaka na Tanzania tunayoifahamu ya watu wenye ukarimu,”alisema.


Alimshukuru Waziri Mkuu pamoja na serikali kwa kutambuamahitaji ya waislamu katika kipindi hikina kuamua kuwasaidia kitoweo kitakachowawezeshakutimiza jambo hilo la maulidi bila shida.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Maulidi litalofanyika jijini Mwanza baada ya sala itakayoswaliwa kwenye viwanja vya Furahisha.

Waziri Mkuu atawasili jijini Mwanza jioni kwa ajili ya shughuli hiyo akiungana na Waislamu wa jiji hilo na Watanzania wengine katika kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...