Na Khadija Seif -Michuzi TV

QUEEN Darleen kaolewa... Na nani?Hilo ndilo lilikuwa swali kwa wanadamu wanaoishi kwenye ardhi ya Mjomba Magu baada ya kuona picha za Queen Darling Darleen akiwa na mumewe wa ndoa Isahaka Mtoro.

Hatimaye wawili hao wameamua kuweka mambo hadharani na wala sio siri tena .Queen Darleen kaolewa kweli na Isihaka Mtoro baada ya penzi la kificho kwa muda mrefu ambapo leo wameona isiwe tabu acha Umma wa Watanzania ujue.  Ndoa ilishafika Sikh kadhaa zilizopita na leo wamekutana kwa ajili ya sherehe ya kufurahia ndoa yao.

Kwa kukumbusha tu Queen Darleen ambaye ni msanii maarufu kutoka Lebo ya WCB na dada wa Msanii mwenye ubora wake kwa sasa Nasseb Abdul a.k.a Diamonda walifunga ndoa katika moja ya msikiti uliopo Temeke jijini Dar es Salaam ambapo watu wachache sana ndio waliopata nafasi ya kushiriki.

Baada ya   ndoa hiyo leo sasa Desemba 12,mwaka huu  2019 wameona usiwe tabu waliodhani ilikiwa Muvi waone kilichofanyika ,hivyo hapo Mbezi Beach bonge la sherehe linaendelea na kuhudhuria na mataa kibao.Hata yule mwanadada machachari Gigy Money naye ameshiriki.Kha!Unashangaa wakati shughuli za mataa lazima wawepo na mstaa wenzao.

Wakati sherehe hiyo ikiendelea Queen Darleen ambaye jina lake halisi ni Mwanahawa Abdul pamoja na mumewe Isihaka Mtoro wamepata nafasi ya kuzungumzia ndoa yao na hiyo ni baada ya kufanyika tukio la Queen Darleen kuvushwa pete hadharani.

Unajua Mumewe Queen  Darleen kasemaje? Ngoja nikupashe upashike,bila wasiwasi Isahaka amesema ameamua kumuoa Mwanahawa baada ya kupata ridhaa na baraka kutoka kwa mkewe wa kwanza,hivyo maneno ya kwamba mkewe wa kwanza hana habari hazina ukweli wowote.

"Kwanza naomba ifahamike sijamuoa Queen Darleen bali nimemuoa Mwanahawa Abdul.Muziki ni kazi yake hivyo siwezi kumkataza lakini nje ya.muziki ni mke wangu wa ndoa halali.Hili la kuoa mke wa pili naomba niseme mimi ni Muislamu na sio dhambi kuoa mke zaidi ya mmoja, tunayoruhusu ya kuoa hadi wake wanne maana Mtume alioa wake saba,amesema.

Kuhusu maneno kuwa ameamua Queen Darleen kwasababu ya mkewe wa kwanza kutokuwa na mtoto,Isihaka Mtoro amesema kuwa mkewe hana tatizo la kutopata mtoto,na ndoa yake na Queen haina uhusiano wowote kuwa ameoa ili kutafuta mtoto kwani mtoto  ni mapenzi ya.Mwenyezi Mungu.

Ndoa raha bwana asikwambie mtu! Queen Darleen alipoulizwa kuhusu kutolewa mke wa pili amejibu kuwa kwanza nakuaminia Isahaka alivyomwambia anataka kufunga naye ndoa lakini hatimaye imekuwa kweli na leo full bata.

Anasema kuwa kuhusu kuwa mke wa pili  hajisikii vibaya na ndoa ni jambo la kheri na kwamba ukiwa kwenye ndoa unakuwa mtu halali wa mtu.Hata hivyo amesema kuwa kwake anajisikia furaha na kwamba hajamlazimisha Isahaka amuoe bali wote wawili wameridhiana law dhati ya mioyo yao.

Alipoulizwa kuhusu mtoto Queen Darleen amejibu kuwa ndoa ndilo jambo la msingi na kupata mtoto ni jambo la majaaliwa ya Allah lakini wakati ukifika wa kupata mtoto watakuwa  naye kwani sio dhambi .

Alipomwambia anataka kumuona ulihisi  mshangaa na hakuwamiani lakini hatimaye ameolewa.mwanzoni alifikiria ukeweza lakini baada naye akaona wenzake ataitwa mke na yeye atakuwa mkewe.

Kuhusu mtoto amesema Darleen na mumewe wamesema mtoto ni jambo la kheri na Mungu akipenda watapa mtoto.

Wakati sherehe zikiendelea kwa upande wake Diamond ameshindwa kuficha furaha aliyonayo baada ya dada yake Queen Darleen kufunga ndoa ambapo amesema kila kaka mwenye dada anatamani kuona dada anaolewa.

Diamond amesema kimsingi wawili hao waishi vuziri kwenye ndoa na kwamba yeye anayependwa na dada yake atampenda. "Dada zangu wakianimbia huyu ndio mwenzangu nami nitakuwa huko huko, hata wakigomba mimi siwezi kuwa na upande wowote kwani ikitokea wakielewana nitakuwa sina cha kufanya zaidi ya kuona aibu,"amesema.

Baba yake Queen Darleen Mzee Abdull Naseeb amesema wamefurahishwa na kitendo cha mtoto wake kufungua ndoa ,na ushauri wake waishi kwenye ndoa kwa maelewano mazuri na kila mmoja kutambua nafasi yake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...