Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeifungia mbio ya “Kigamboni International Marathon” kwa muda wa mwaka mmoja, baada ya kufanyika kwa mbio hiyo tarehe 1 Disemba, 2019 bila kufuata Sheria na kanuni za uendeshaji wa mbio za Marathoni.

Muandaaji wa mbio hizo anatakiwa kuhakikisha anakamilisha kulipa zawadi alizotakiwa kutoa katika mbio hizo kabla ya tarehe 12 Disemba, 2019.

BMT kupitia Kaimu Katibu Mkuu, Neema Msitha, amesema kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la uandaaji za Marathoni pamoja na mbio nyingine za barabarani nchini, ambapo zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuendeleza mchezo wa riadha pamoja na kukuza uchumi nchini.

Amesema, hata hivyo pamoja na mchango mkubwa; kumekuwa na changamoto nyingi za uendeshaji wa mbio hizo zikiwemo baadhi ya waandaji kuandaa mbio bila kusajiliwa, kukosa ulinzi barabarani (traffic control), kukosekana kwa huduma za afya (ambulances).

Msitha amesema pia mbio hizo zimekuwa zinakosa huduma ya maji ya kunywa katika vituo vya kukimbilia pamoja na baadhi ya wandaaji kushindwa kulipa zawadi kwa washindi, kukosa wataalam/wasimamizi wenye weledi, jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa udanganyifu.

Ameeleza, kushindwa kukamilisha taratibu zote zimekuwa zinasababisha Changamoto ambazo zimepelekea mgogoro mkubwa baina ya wandaaji, washiriki wa mbio hizo (wakimbiaji) pamoja na wadau wengine wa mchezo wa riadha.

BMT wasema, kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo kuanzia tarehe 1 Januari 2020, vibali vyote vya kuendesha mbio za Marathoni na mbio nyingine za Barabarani ngazi ya Taifa, mkoa na wilaya vitatolewa na Baraza la Michezo la Taifa baada ya kupitiwa na Shirikisho la Riadha Tanzania. 

Vibali hivyo vitatolewa baada ya Baraza kujiridhisha kuwa muandaaji wa mbio hizo amekidhi matakwa ya uendeshaji wa mbio hizo.

Aidha BMT limezielekeza mamlaka za usimamizi wa Michezo ngazi ya Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa hamna mbio yoyote ya barabarani inafanyika bila kibali cha BMT.

Kwa mujibu wa Sheria ya BMT waandaji wote wa mbio hizo wanapaswa kulipia asilimia moja (1%) ya tiketi/viingilio vya mbio, kwenda katika mfuko wa maendeleo ya Michezo BMT,Vilevile kuanzia leo tarehe 3 Disemba 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...