MKUU wa Chuo cha Ustawi  wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amefungua Kongamano la saba la  kitaaluma ambalo lilijadili mageuzi ya ajenda ya uchumi wa viwanda na uhitaji wa ushirikishwaji wa karibu wa Jamii katika mageuzi hayo ili kufanikisha azma hii kubwa ya nchi.

Ni utamaduni  wa vyuo vya elimu ya juu kufanya kongamano la kitaaluma kabla ya mahafali ya Chuo ambapo kongamano hilo hujumuisha wahadhiri, wahitimu, na wanafunzi wa chuo kujadili na kuchangia mada hiyo kwa manufaa ya mabadiliko ya kitaaluma ya chuo na nchi.

Prof. Wetengere Kitojo aliyekuwa mwezeshaji Mkuu wa mada hii ameainisha masuala muhimu ya kuzitangia ili kuhakikisha vyuo vya elimu ya juu vinasaidia nchi katika kufanikisha jamii kuwezeshwa kushiriki  katika mageuzi ya uchumi wa viwanda.

Prof. Kitojo amesema kuna haja kubwa kwa sasa kwa vyuo kuangalia mitaala yake na ufundishwaji wa wanafunzi,  ili viweze kumuandaa mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujiari au kufungua viwanda, pia vyuo kutoa elimu isiyo rasmi ya viwanda kwa jamii alitaja kama jambo muhimu vyuo kufanya ilikuwezesha ushiriki wa wananchi katika uchumi wa viwanda.

Aliongeza na kusema hii itatoa nafasi kwa uchumi wa viwanda sio tu kubadiilisha tarakimu za mapato ya nchi bali pia mabadiliko ya maisha ya watu wote na jamii kwa ujumla.

"Tunahuitaji mageuzi ya uwekezaji wa viwanda ambapo tutaona soko la ajira na vibarua kwa watanzania likiongezeka na sio uwekezaji mkubwa wa fedha nyingi ambao hauna fursa za ajira kwa watu wetu". alisema Prof. Kitojo.

Chuo cha Ustawi wa Jamii kinafanya mahafali ya arobaini na tatu leo katika viwanja vya chuo hicho kijitonyama Dar es Salaam ambapo kinatarajia kuwatunuku wahitimu takriban 1300  katika ngazi mbali mbali za elimu.
Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akifungua Kongamano la Saba la Kitaaluma Jana Chuoni hapo
Prof. Wetengere Kitojo akiwasilisha mada kwa wanataaluma kwenye kongamano la saba la Chuo cha Ustawi wa jamii jana Chuoni hapo Kijitonyama Dar es Salaam.
Wahitimu na wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wakifuatilia mawasilisho katika kongamano la Saba la Chuo hicho lilifanyika jana chuoni hapo Kijitonyama Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...