Na Farida Saidy, Morogoro 

Jamii imetakiwa kuachana  na biashara haramu za madawa ya kulevya na kugushi  nyaraka za serikali badala yake kufunya  shughuli halali ambazo zinaweza kuwaingizia kipato hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka

Rai hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilboad William Mutafungwa ofisini kwake, baada ya watu tisa kukamatwa kwa makosa tofauti yakiwemo kusafirisha madawa ya kulevya aina ya bhangi na kugushi nyaraka za serikali pamoja na wizi wa vitu vya thamani zikiwemo runinga.

"Jeshi la polisi mkoa wa morogoro tunawashikilia watu tisa kwa matukio mbalimbali ya uharifu pia tumefanikiwa kukamata bhangi gunia 6, kg 6 na kete 50 ya bhangi, roli lililokuwa likisafirisha bhangi, TV 08, Computer 02 na pia tunaendelea na uchunguzi wa matukio mbalimbali ya jinai yaliyojitokeza..."  alisema kamanda Mutafungwa. 

Ameeleza kwamba  mnamo tarehe  30/11/2019 majira ya 00:30 katika kijiji cha dala kata na tarafa ya mvuha askari polisi wakiwa doria wamefanikiwa kuwakamata wasafirishaji bhangi kwa kutumia roli aina ya fuso lenye namba T.671 CPM.

Aliwataja wasafirishaji hao kuwa ni Respice Joachimu dereva,  utingo wake Iddi Boga, Abdalla Azizi dereva bodaboda wote wakiwa wakazi wa manispaa ya Morogoro,ambapo walikuwa wakisafirisha bhangi hizo ndani yake kukiwa na mfuko wa pumba za mpunga.

Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amesema kuwa wanamshikiria  mkurugenzi wa kampuni ya MOROSIGN, Bwana omari Kassim Mataka na Bwana Mussa Salim Mshana afisa masoko wa kampuni ya SUPER TECH ENTERPRISES   kwa kosa la kukutwa na vifaa vya kugushi nyaraka za serikali zikiwemo za TRA na TANESCO

Kamanda Mutafungwa amewataka Watanzania kuachana na imani za kishirikina baina yao badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona kuna walakini katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...