Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake 

MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda kulia akimkabidhi kitabu hicho Samweli mara baada ya kufanya uzinduzi
MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso kushoto akimpatia nakala ya kitabu kilichoandikiwa na Mwanae Mtangazaji wa Kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM Radio Dkt Isaac Maro wakati wa uzinduzi huo 
Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake na mdogo wake Alan Michael Gimeno 

Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) katikati akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa kitabu chake

Jumamosi tarehe 7/12/2019 ilikuwa siku ya pekee wa mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) ambae alibahatika kuzindua kitabu chake cha kwanza ndani ya fursa ya Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Center 

Kitabu cha BIBLIA YANGU kilizinduliwa na Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda 

Samwel amekuwa mtoto wa pekee kwenye familia ambae Mungu Ameweka kipaji cha kuandika na kuchora na Sisi kama wazazi wake tumeamua kumsaidia ili kuiishi ndoto yake maneno hayo yamesema na mama mzazi wa Bi Suzana Senso

Kitabu cha kwanza cha Samwel kitakwenda Kuwa kinatolewa kwa watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya samwel kurudisha kwa watoto wezake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao ni mara chache sana kupata kitabu kinzuri na chenye hadithi za kwenye Biblia kutokana na mazingira wanayoishi maneno hayo yamesemwa na baba wa Samwel Bw Michael Samwel Gimeno 

KAMPENI KALAMU YANGU
Ni maneno yatakayo kwenda kutumika kwenye kampeni samwel ambayo itakuwa nikutembelee vituo vya watoto yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuwagawia vitabu ili nao waweze kusoma sio tu kusoma kitabu tu ila pia kusoma kitabu kilichoandikwa na mtoto mwezao 

Kampuni hii inaanza mwezi huu wa 12 hadi siku ya wapendanao tarehe 14/2/2020 ambapo samwel atakwenda kula na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambacho tutakitaja siku zijazo na pia kuwagaia vitabu ya BIBLIA YANGU 

Gharama ya kitabu itakuwa shilingi elfu 20,000 kuanzia 15/2/2020 baada ya kampuni ya KARAMU YANGU ukisha tarehe 14/2/2020

Mama Samwel alisema Kwa sasa tunatamani kupata watu wa ku support kutoa nakala ya vitabu ambavyo tunatajia kuvigawa kwenye vituo vya watoto yatima Kwani hii kampeni haina mfadhili wa kufanya Ila ni wazazi tu  ndio tunaifanya na tunatamani kuwafikia watoto wengi sana 
Kwa yeyote atakae wiwa kuungana nasi kwenye Hii kampuni anaweza ku wasiliana Kupitia namba 0736 372138 

Tukiwa kama wazazi wa Samwel tunapenda kuwashukuru Joel Kiiya ambae ni mentor wa Samwel, Bi Ezabel Simuyu ambae ndie ame design kitabu, photography wake Muki, Emanuel, Mkurungezi wa Fursa na wale waliotumia muda wao kufanikisha kitabu cha “BIBLIA YANGU” hadi kutoka.


MUNGU AWABARIKI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...