Viongozi wa vyama tisa(9) vya Ushirika vya Msingi vya mazao (AMCOS ) katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga wamepatiwa mafunzo ya kukuza njia asilia za kilimo ili kuwa saidia wakulima kuongeza ubora na kuhakikisha kunakuwa na kuhakikisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye kwa mtumiaji yeyote.

Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Ukumbi wa WALIOCHONACHO NA WASIOKUWANACHO uliopo Mtaa wa Ruhuwiko Mjini Mbinga yaliyotolewa na Kampuni ya Kahawa ya Starbucks yenye makao yake makuu jijini Mbeya na lengo lamafunzo hayo ni kukuza njia asilia za kilimo cha kahawa, ili kuwasaidia wakulima kuboresha zao la kahawa, na kuongeza ubora na kuhakisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye

akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa Idara ya kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bw.Menance Ndomba alisema Halmashauri ya Wilaya ya Nyasaitawachukulia hatua kali maafisa kilimo wote ambao hawatawasaidia wakulima kuongeza ubora wa kahawa ili kuwapa maendeleo wananchi.

Bw. Ndomba amefafanua kuwa atahakikisha Maafisa kilimo wote Wilayani Nyasa, ambao watashindwa kuwapa elimu wakulima ili wazalishe kahawa yenye ubora atahakikisha anawachukulia hatua za kinidhamu pamoja na kuwafukuza kazi.

Aliongeza kuwa kahawa ni zao la kimkakati ambalo Serikali imelipa kipaumbele hivyo maafisa kilimo wanatakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuwapa elimu wakulima na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuzalisha kahawa yenye ubora na nyingi na kupelekea wananchi wanapata maendeleo.

“Maafisa kilimo wa Wilaya ya Nyasa nitawapima kwa kuangalia wananchi wamepata ubora gani wa kahawa. Afisa kilimo mmeajiriwa kwa kazi ya kuhakikisha wananchi/wakulima wanakuwa na maendeleo kwa kuzalisha mazao yenye ubora na yakutosha.Tunapozungumzia maendeleo ni pamoja na kuhakikisha Wakulima wanakuwa na elimu ndelevu ya mazao mbalimbali hasa mazao ya kimkakati. Nichukue fursa hii kuwaambia Nyasa hatumtaki Afisa kilimo asiyetoa elimu kwa wakulima wake ili waweze kuzalisha mazao bora.

Aidha bw.Ndomba ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha na kusimamia mfumo wa Vyama vya Msingi vya Ushirika vya Mazao (AMCOS) kwa kuwa wakulima wameweza kuuza kahawa zao kwa pamoja kwa bei mzuri, kuweza kufanya manunuzi ya Pembejeo kwa pamoja (Bulk purchase) hususani mbolea ambapo AMCOS zilizopo Nyasa tayari zimeshanunua mbolea na kusambaza kwa wanachama wake.

Naye Meneja wa Kampuni ya Stabucks Farmers Center amesema kahawa inayotoka Wilaya ya Mbinga na Nyasa ni nzuri na inapendwa katika soko la Dunia kwa kuwa ni ya asili, hivyo tunatakiwa kuongeza ubora wa kahawa yetu na kuulinda ili bei iwe nzuri, mkulima anufaike zaidi kwa kuuza bei ya juu kwa kuwa ubora wa kahawa unaongeza Bei katika soko la Dunia.

Aliwapongeza wakulima hao kwa kazi nzuri ya kuzalisha kahawa nzuri, na kuwataka kuongeza uzalishaji wa kahawa inayolimwa katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga.

Mafunzo haya ni ya siku moja yaliyowakutanisha Viongozi wa vyama vya msingi vya wakulima wa kahawa,vya Tingi,Upolo,Luhangarasi,Kingerikiti,Nambawala,Mapendo na Lipo kwa Wilaya ya Nyasa na Ngaka na Mahenge kwa Wilaya ya Mbinga, Maafisa kilimo na wadau wa zao la kahawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...