Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwasalimia wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiongea wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Asas Super League 2019/2020 hatua nane bora imemaliza hatua ya mzunguko wa tatu kwa timu ya mafinga academy kuongoza kundi B na Isiman Fc kuongoza kundi A huku timu ya mafinga academy wakiongoza kwa kufunga magoli kumi.


Kufuatia kutamatika kwa mzunguko wa tatu wa Asas Super League 2019/2020 kundi Alinaongozwa na timu ya Isimani fc yenye alama saba na magoli ya kufunga matano huku ikiwa imefungwa goli moja tu katika michezo mitatu ya awali.

Kidamali fc na kalinga fc wanalinga alama kwa kila timu kwa kuwa na alama nne huku wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Kidamali fc akiwa na magoli ya kufunga matano na wamefungwa magoli mawili tu na timu ya kalinga wakiwa wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne.

Timu ya Young Stars wakiwa wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa wana alama moja huku wakiwa wamefungwa jumla ya magoli sita katika michezo mitatu waliyocheza katika mzunguko wa kwanza wa Asas Super League 2019/2020

Kwa upande wa kundi B,timu ya Mafinga Academy wanaongoza kundi B wakiwa wamekusanya jumla ya alama tisa huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa wamefunga jumla ya magoli kumi na kufungwa magoli mawili kwenye michezo mitatu ya awali ya kundi B.

Timu ya Mkimbizi fc,Nzihi fc na Irole Fc zote zimekusanya jumla ya alama mbili kwenye michezo mitatu huku wakiwa wametofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa,ukiangalia Mkimbizi Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli matatu,Nzihi fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne na Irole Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli saba na ndio timu inayongoza kwa kufungwa magoli mengi kuliko timu yeyote ile kwenye hatua ya nane bora.

Asas Super League 2019/2020 itaendelea siku ya ijumaa tarehe sita mwenzi wa kumi na mbili kati Kidamali Fc na Isimani fc mchezo utachezwa katika uwanja wa Kidamali na ikumbukwe kuwa kwenye nmchezo wa awali timu ya Isimani ilishinda kwa goli moja bila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...