Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Nyota wa Kimataifa wa Argentina na Klabu ya Soka ya Barcelona ya Hispania, Lionel Messi rasmi ametangazwa kuwa Mshindi wa Tuzo ya Ballon d'or ikiwa ni mara ya 6 kutwaa Tuzo hiyo akiwa ni Mchezaji wa kwanza duniani kuchukua kwa idadi hiyo katika historia ya Soka.

Messi ametwaa tuzo hiyo inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka nchini Ufaransa akitwaa mwaka 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019.

Katika Tuzo hizo zilizotolewa mjini Paris nchini Ufaransa, Nyota wa Kimataifa wa Marekani kwa upande wa Wanawake, Megan Rapinoe ametajwa katika Tuzo hiyo ya Ballon d'or kwa mwaka huu wa 2019.

Matthijs de Ligt wa Uhoalanzi na Klabu ya Juventus ametajwa katika Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana (Kopa Trophy 2019) wakati Jadon Sancho wa Borussia Dortmund akitajwa kwenye nafasi ya Pili na Joao Felix wa Atletico Madrid akitajwa katika nafasi ya tatu.

Golikipa wa Kimataifa wa Brazil na Klabu ya Liverpool, Alisson Becker ametajwa kuwa Kipa Bora wa Tuzo ya maalum iliyopewa Jina la Yachine Trophy 2019.

Wachezaji 3 kutoka Bara la Afrika waliingia katika 10 Bora zakuwania Tuzo hizo za Ballon d'or ambao ni Riyad Mahrez, Sadio Mane na Mohammed Salah, wakati huo Mane ametajwa katika nafasi ya Nne baada ya Mshindi kupatikana ambaye ni Lionel Messi. 

Sherehe za Utoaji Tuzo hizo zilishereheshwa na Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Ivory Coast na Klabu ya Chelsea, Didier Drogba na Mwandishi wa Habari wa Ufaransa, Mwanadada Sandy Heribert.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...