Amos Ndyagumanawe kutoka Nchini Uganda amefuzu kushiriki mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Pool yajulikanayo  “Chines 8 Ball WeMasters Championship 2020” yanayotarajiwa kufanyika Qinhuangdao City Nchini China Januari 3 – 8,2020 kwa kushirikisha Mataifa 42.
Amos alifuzu nafasi hiyo katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Whisky River  Nairobi nchini Kenya kwa kushirikisha nchi tatu yaani Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya na kwa kufuzu huko alizawadiwa pesa taslimu za Kenya shilingi 200,000/= sawa na milioni 4,478,721.73 za Kitanzania, Saa ya Ukutani ya kisasa inayoashilia mchezo swa Pool,Ticket ya Ndege ya kwenda na kurudi nchini China pamoja na huduma zote za chakula na maladhi.
Amos ataambatana na Mchezaji mmoja kutoka Tanzania, Amos Boniphace ambaye ni mlemavu wa mkono na mguu aliyepewa nafasi ya upendeleo kushiriki mashindano hayo nchini China kwa ufadhili wa Uongozi wa Chines 8 Ball wa nchini Kenya.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Joseph Kasozi pia kutoka Uganda ambaye alizawadia pesa taslimu za kikenya shilingi 100,000 sawa na shilingi milioni 2,239,360.87 za Tanzania, mshindi wa tatu ni Morgan Muema kutoka Kenya ambaye alizawadiwa pesa taslimu za Kenya shilingi 50,000 zawa na milioni 1,119,680.43 za Tanzania, mshindi wa nne ni Baraka Jackson kutoka Mkoa wa Mayara nchini Tanzania ambaye alizawadia pesa taslimu za Kenya 30,000 zawa na shilingi 6,71,808.26 za Tanzania,mshindi wa tano mpaka wa nane walizawadiwa pesa taslimu za kesha shilingi 10,000 ambazo ni sawa na 2,23,936.09 za Tanzania ambao ni Simoni Lubulwa kutoka Uganda, Caesar Chandiga kutoka Uganda, Collins Tuwei kutoka Kenya, AlfredGumikiriza kutoka Uganda.
Mshindi wa tisa mpaka kumi na sita walizawa pesa taslimu ya Kenya shilingi 5,000 sawa na shilingi 1,11,968.04 ya Tanzania ambao ni Stephen Kyalo kutoka Kenya, Bwanika Mansoor kutoka Uganda, John Kyalo kutoka Kenya, Henry Mwangi kutoka Kenya, Lucas Mbugua kutoka Kenya, Geoffrey Setumba kutoka Uganda, Kituku Munguti kutoka Kenya na  David Njane kutoka Kenya.
Mashindano hayo yalijumuisha jumla ya Wachezaji 64 kutoka nchi hizo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Wachezaji waanne ambao ni Abdallah Hussein(Dar es Salam), Ahmed Sahil(Dar es Salaam), Amos Boniphace(Dar es Salaam) na Baraka Jackson(Manyara).
Akizungumza na Wachezaji pamoja na waandishi wa habari,Mratibu wa mashindano ya Afrika Mashariki, Peter Kinyua kwanza aliipongeza kamati ya maandalizi iliyoendesha mashindano kwa ushumla mpaka kumalizika kwa usalama, pili aliwapongeza wachezaji wote walijitokeza kushiriki mashindano hayo ya funga mwaka 2019, lakini zaidi aliwapongeza washindi wote waliopata zawadi  na zaidi alimpongeza Bingwa, Amos Ndyagumanawe kwa ushindi na kumuomba ajiandae vyema sasa kuwawakilisha wana Afrika mashariki kwanye fainali za Kimataifa Nchini China hapo Januari 2020.Lakini pia aliwaomba wapenzi na wadau wote kwa sasa tuelekeze hakili na masikio yetu kwenye fainali za Kimataifa zijulikanazo kama “Chines 8 Ball WeMasters Championship 2020” zinazo tarajiwa kuanza Januari 3-8,2020.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...