Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe leo amejumuika na viongozi wengine wa vyama na serikali kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Hii ni mara ya kwanza kwa viongzoi wa chama hicho kikuu cha upinzani kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo ambazo pia zilihidhuriwa na Mbunge wa Kibamba jijini Dar es Salaam Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mhe. Joseph Mbilinyi aka Sugu, Mbunge wa Tarime Mhe. John Heche,  pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

 Mstahiki Meya wa Ubungo Mhe. Boniface Jacob naye alitinga uwanja wa CCM Kirumba  akiwa naye amevaa sare zao za magwanda.

Wabunge hao kama ambavyo ilivyo kwa viongozi wengine wa kisiasa walioshiriki sherehe hizo walipata nafasi ya kukaa jukwaa kuu kushuhudia kila kinachoendelea uwanjani hapo.


Viongozi wa Chadema kwa muda mrefu walikuwa wamesusia kushiriki sherehe hizo lakini bikla shaka safari hii wameona isiwe taabu. Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana naye alikuwa miongoni mwa walioshiriki.

Wakati huo huo mbali ya wabunge hao, pamoja na wabunge wengine lukuki wa CCM walioshiriki katika sherehe hiyo, idadi kubwa ya wananchi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani nao wamejitokeza kwa wingi,Idadi ya watu ilikuwa kubwa kiasi cha Rais Dk.John Magufuli kueleza watu waliojitokeza ni wengi sana na haijapata kutokea kuona kuna viongozi wa kada zote na kwa awamu tofauti.

Ukweli ni kwamba hamasa ya wananchi wa Mwanza kushiriki kwenye sherehe hizo ni kubwa na mapema kabisa ilionekana namna ambavyo makundi ya watu yalivyokuwa yakipita mtaani kuelekea CCM Kirumba.

Katika kuhakikisha watu wanapata nafasi ya kuingia uwanjani mapema, milango ilikuwa imefunguliwa saa 10 alfajiri na hivyo kutoa nafasi kwa kila aliyekwenda kutotumia muda mwingi kupanga foleni ya kuingia uwanjani hapo.

Ilpofika saa moja asubuhi karibu majukwaa yote ya uwanjani hapo yalikuwa yamejaa na wakati huo huo watu wakiendelea kuingia kwa kupanga foleni.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa idadi kubwa ya watu kujitokeza uwanjani hapo ni mapenzi ya Watanzania kwa Serikali na Taifa lao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...