KATIKA kuhitimisha mkutano Mkuu wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) bodi hiyo imetoa tuzo kwa taasisi, makampuni na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018.

Akizungumza wakati wa ufungaji na utoaji wa tuzo hizo wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shabani amesema kuwa maadili na Uhasibu ni muhimu katika kuutumikia umma wa Tanzania.

Amesema, tasnia hiyo inahitaji uaminifu wa hali ya juu hasa katika kufanya maamuzi pamoja na mipango inayolenga taifa kwa ujumla.

"Ni matumaini yangu kuwa siku hizi tatu mlizokaa na kujadili masuala yahusuyo sekta hii yataleta manufaa kwa jamii, nawasihi mkaendeleze na kutekeleza tuliyoyajadili"

Aidha amesema kuwa katika kufikia azma ya kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025 sekta hiyo ina mchango mkubwa na wenye tija kwa jamii.

Pia amezipongeza taasisi, makampuni na mashirika yaliyofanya vizuri na kutunukiwa tuzo na kuwashauri waendelee kuonesha juhudi hizo ili kuipeleka nchi mbele zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu  (NBAA) CPA Profesa Isaya Jairo amesema,sekta hiyo imeendelea kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji na hiyo ni pamoja na kutoa tuzo kwa taasisi na mashirika yaliyofanya vizuri ili kuleta chachu kwa mashirika mengine.

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeendelea ushirikiano wa hali ya juu na kupelekea tasnia hiyo kufahamima Kimataifa.

Akieleza  kuhusu tuzo hizo Prof. Jairo amesema kuwa kila mwaka katika mkutano mkuu wamekuwa wakitoa tuzo hizo ambazo zimekuwa zikuhamasisha uwajibikaji na uwazi kwa kizazi cha Sasa na baadaye.

Taasisi zilizochukua tuzo hizo ni TBL, TCC na Tanga Cement ambayo imeshika nafasi ya kwanza, Taasisi za elimu ambazo zilizochukua tuzo hizo ni Taasisi ya Ustawi, Chuo kikuu Mzumbe na chuo Cha kilimo SUA.

Mashirika mengine yaliyoibuka na ushindi ni pamoja na  AICC, TANAPA, TANAPA, TBC, TCCAA, TRA, DSE, CMC, Swis Port pamoja na Benki za kati ambazo ni City Benki, Mkombozi Benki na DCB huku Barclays, NMB na CRDB wakiibuka vinara kwenye kitengo cha Benki.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo pamoja na kutoa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo akizungumza akitoa historia fupi ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mgeni rasmi pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo pamoja na utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango,  Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni(kulia) tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha Vyuo Vikuu katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango,  Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka tuzo ya mshindi wa Pili kwenye kipengele cha Vyuo Vikuu katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Bi.Renatha Ndege ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Edwin Mhede mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo kwa Viongozi mbalimbali wa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika yaliyofanya vizuri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  
Baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  washindi wa Tuzo za uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...