SERIKALI ya Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mikakati mahsusi ya kuimarisha na kuendeleza sekta ya viwanda ili kuongeza ajira na kuwapunguzia umaskini kwa wananchi wake huku kusisitiza kuendelea kuwalinda wawekezaji wote wanaoamua kuanzisha viwanda hapa nchini kwa kuwapatia vivutio maalumu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira muafaka ya uwekezaji na biashara.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere.

“Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa bidhaa zisizo na viwango na bandia hazitakuwa na nafasi katika soko la Tanzania, hivyo ni muhumi kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na viwango vya kimataifa ili kuvipa changamoto viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa zenye ubora” amesema Mhe Mhandisi Manyanya

Ameendelea kuwaomba wawekezaji kuendelea kuwekeza Tanzania kwasababu ina maeneo mazuri ya kujenga viwanda, fursa za malighafi na kuna walaji wa kutosha kwasababu Watanzania wapo takriban million hamsini na tano hivyo kuna soko kubwa la bidhaa zao.

Ameendelea kusema kuwa, serikali ya Tanzania imeshatambua na kufahamu umuhimu wa mazingira wezeshi kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa viwanda, imechukua jukumu la kuweka miundo mbinu wezeshi kwa kuhakikisha kwamba umeme unapatikana."Ndio maana tunajenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji takriban megawat 2500 lakini vilevile kuna umeme ulioongezwa pale Kinyerezi na kuchangia ongezeko la takriban megawatt 1600 na kufanya nchi yetu kuwa na umeme wa kutosha hivyo kiwanda kinaweza kuanzishwa sehemu yoyote."

Pia amesema Serikali imeendelea kuondoa mikanganyiko ya kodi na mikanganyiko ya taasisi za udhibiti kwa kuhakikisha kuwa inapunguza kodi na mpaka sasa kodi takribani 168 zimeondolewa kwaajili ya kuweka mazingira wezeshi na Mamlaka nyingi kama vile Taasisi ya Tume ya Ushindani (FCC) na nyingine zote zinazohusika na ukaguzi zinazingatia bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa bidhaa halisi na haziui soko la ndani.

Ameongeza kwa kueleza kama ambavyo ilivyo kwenye dira ya Taifa, ifikapo 2025 tunatamani kuona Tanzania inafikia uchumi wa kati lakini kufikia hapo ni pale taasisi za serikali zitakapokuwa na msimamo mmoja kuhakikisha kwamba tunaisaidia sekta binafsi ambao ndio watekelezaji na watendaji katika uzalishaji na kuwezesha upatikanaji wa uzalishaji wenye tija na kufanya bidhaa zetu ziwe na bei zinazoweza kumfikia mlaji na hivyo kukuza uchumi wetu.

Ametoa rai kwa wadau na washiriki wanaoonesha bidhaa zao kuhakikisha kila wanachozalisha wanazingatia ubora unaostahili na amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) kufadhili mradi wa kuunda kanzidata ya viwanda vinavyoanzishwa na vinavyokuwa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Dkt Stephen Kargbo ambaye ni Mwakilishi wa UNIDO nchini Tanzania amesema kuwa uwepo wa siku ya viwanda vya ndani ni muhimu kwani hufanya kujua changamoto ambazo watu wenye viwanda wanakutana nazo na ni fursa kwa wadau kubadilishana mawazo kuhusu viwanda na njia bora za kutumia jambo ambalo linaloakisi ukuaji na ushirikiano katika nchi za Afrika.

Ameongeza kwamba katika kuendeleza muingiliano wa kibiashara katika nchi ya Afrika soko la pamoja la AFCFTA linatarajiwa kuongeza ushindani na kusisimua sekta ya uzalishaji

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania Dk.Ng’wanza Kamata amewashukuru washiriki wa Maonesho hayo kwa kuitikia wito wa kuja kushiriki na amesema kuwa uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza ujenzi wa uchumi wa viwanda hivyo iwe agenda ya kuduma hadi nchi itakapo simama imara katika ujenzi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Viwanda na Bishara Mhandisi Stella Manyanya akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika leo Desemba 7 mwaka 2019 ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati ya Serikali kuboresha mazingira ya biashara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...