TAASISI ya kutetea masuala ya ukatili wa kijinsia (PHLI) ya Dar es salaam kwa kushirikiana na jeshi la polisi wameazimia namna ya kuifikia jamii katika kuipa uelewa dhidi ya vitendo vya rushwa ya ngono ambavyo vimeongezeka kwa watoto na wanawake.

Mjadala huo uliofanyika katika kituo cha polisi kati Dar es salaam kiliibua hoja mbalimbali kwa washiriki katika kukomesha na kutokomeza ukatili wa kijinsia ambapo maazisho yalianza novemba 25 hadi kilele chake disemba 12 mwaka huu.

Akizungumza katika kikao hicho mtaalamu kutoka taasisi ya Prosperous health life initiative (PHLI) wakili Hilda Dadu alisema inapaswa kuwa na mijadala ya pamoja kati ya asasi na jeshi la polisi namna ya kuwafikia wananchi kwa kuwapa uelewa wa matukio ya unyanyasaji yatokanayo na rushwa ya ngono.

"Vyombo hivi vinatakiwa vikutane pamoja kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuweza kuifikia na kuielimisha jamii kuhusiana na matukio ya kikatili yanayofanywa na baadhi ya watu," alisema Dadu

Dadu amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio yatokanayo na rushwa ya ngono  katika maeneo ya kazi,  mashuleni, mavyuoni na hata kwenye vituo vya afya yanayofanywa na baadhi ya watu kuweza kujinufaisha kimwili.

Kwa upande wake RPO wa mkoa wa kipolisi ilala Emmanuel Pango amesema kuwa chanzo kikubwa cha rushwa ya ngono inatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii na kufanya mdogo kuto muheshimu mkubwa na mkubwa kuto muheshimu mdogo.

Amesema kuwa kwa umoja wanatakiwa kuifikia jamii kwa kuiambia na kuihakikishia kuwa matendo maovu yatokanayo na rushwa ya ngono yanaweza kuepukika kwa wahusika kuweza kuchukuliwa hatua stahiki baada ya tukio kutokea.

Aliendelea kwa kusema suala la rushwa makazini ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika wala halikubaliki ndani ya jamii hivyo basi kila mmoja anatakiwa kuwa makini kwa kulitolea taarifa kwa haraka kwenye  madawati ama vituo vya polisi ama vya kisheria.

Naye kamishna msaidizi mnadhimu namba moja katika mkoa wa kipolisi Ilala Janeth Stephano amesema kuwa mjadala huo uwe ni muendelezo wa kuchukua hatua za kuifikia kwa kuipa uelewa wa kutosha kwa minajili ya kupunguza na kutokomeza masula ya ukatili na rushwa ngono kwa Watoto na wanawake.

Kikosi cha jeshi la polisi pamoja na wanaharakati wa masula la kupinga ukatili wa kijinsia mara baada ya kumaliza kikao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...