Taasisi ya Ustawi wa Jamii imenyakua nafasi ya kwanza na kupata tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla iliyofanyika Disemba 7, jioni katika viwanja vya NBAA Bunju.

Kwa mara ya nne mfululizo Taasisi ya Ustawi wa Jamii inashiriki na Kunyakua ushindi kwenye tuzo hizi muhimu katika taaluma ya Uhasibu Tanzania.

Akiongea baada ya Kupokea tuzo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amesema ni furaha kubwa kwa Taasisi kutunukiwa tuzo hii ambayo ni kielelezo cha weledi na umahiri wa hali ya juu wa utunzaji wa taarifa za fedha na menejimenti nzuri za fedha za serikali katika Taasisi Yetu.

"Tumekuwa tukitoa huduma ya taaluma ya elimu, na ni manguli wa kutoa na kufundisha katika taaluma ya ustawi wa Jamii lakini sasa tunaonyesha weledi mkubwa katika fani ya uhasibu na utunzaji taarifa za fedha, naipongeza sana timu yangu ya Uhasibu ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiongozwa na CPA Athuman Senzota." alisema Dkt. Joyce.
 Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akipokea Tuzo ya Mshindi wa Kwazna ya uandaaji taarifa za fedha kwa mwaka 2018 katika kundi la Vyuo vya elimu ya Juu,
 Kutoka Kushoto Dkt. Joyce Nyoni Mkuu wa Taasisi, Dkt. Zena Mabeyo Kaimu mkuu wa Taasisi fedhaUtawala, CPA Aisha Kapande Mhasibu,CPA Manase Shunashu Mhasibu, Na nyuma CPA Athman senzota Mhasibu Mkuu 
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na timu yake wakifurahia ushindi wa Tuzo ya kwazna ya Uandaaji wa taarifa za fedha 2018
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...