Na Charles James, Michuzi TV, Dodoma

Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya JUAN, inayotekeleza mradi wa Maji wa Kelema Kuu, katika Kijiji Cha Kelema Balai Wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, kuhakikisha ndani ya siku kumi mradi huo uwe umekamilika.

Awali mradi huo ulioanza kutekelezwa tokea 2014 wenye thamani ya sh mil 223 ulikamilika lakini ulifanya kazi ndani ya wiki moja kutokana na mabomba yaliyowekwa yalikuwa chini ya kiwango.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo wameamua kutoa siku hizo ili kusaidia wananchi wa kitongoji cha Ndoroboni kilicho ndani ya kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba wapate maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

"Tumetoa siku hizo kwa wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo,hatutaki visingizo kwa sababu mitaro tayari imeshachimbwa,"alisema Kibwengo.Alifafanua kuwa wanatakiwa kwenda kwa kasi katika uwekeaji mambomba hayo.ili kukwepa tope kuyafukia kutokana na kwamba msimu wa mvua umeanza.

Akitoa ufafanuzi baada ya kufanya uchunguzi wao amesema walichokibaini ni kwamba mambomba yaliyonunuliwa kuweka katika mradi huo yalikuwa na kiwango chenye presha ya kawaida (Normal Presha)PN 6 badala ya PN 12.5 kama ilivyoidhinishwa katika mkataba wa kutekeleza mradi huo.

Kutokana na hilo amesema siku hizo walizotoa hakutakuwa na msamaha wowote kwa kampuni hiyo kwasababu ni uzembe na udanganyifu uliofanywa na mkandarasi huyo katika mradi huo,kinachotakiwa ni wao kufanya kazi haraka iwezekanavyo hasa ukizingatia mitaro tayari imechimbwa.

Naye Mhandisi wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilayani Chemba Robert Mganga amesema kazi iliobakia ni nyepesi sana hivyo wiki moja inatosha kukamilisha kufanya utandikaji huo wa mabomba.

"Hakuna kazi ngumu hapa sema hii kampuni inaleta uzembe,tuko nao pamoja hivi sasa kuhakikidha wanakamilisha ujenzi wa mradi huo,"amesema Mganga.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Ndoroboni amesema kitongoji hiko kina shida ya maji inayopelekea wakazi wa eneo hilo kuafuata kijiji cha Kelema Balai kama maili mbili kutoka Kelema Kuu.

Hata hivyo ameiomba serikali kwa kishirikiana na serikali ya mtaa kusimamia mradi huo ukamilike ili wakazi waweze kupata maji safi kwa ajili ya matumizi ya kila siku.Amesema wakazi wengine hushindwa kwenda umbali mrefu na badala yake wanatumia maji ya mabwawa ambayo ni machafu na si salama kutumia kwa binadamu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kampuni ya Juan Mhandisi Inocent Benard amesema wakazi wa eneo hilo wategemee mwezi huu kupata maji kutokana na kuwa watakamilisha ndani ya siku ambazo wametakiwa kukamilisha.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Bw. Sosthenes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...