Na Andrew Chale, Bagamoyo

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ipo mbioni kukamlisha ujio wa progamu mpya za kozi mahasusi zitakazosaidia ukuaji wa Sanaa, urithi wa Utamaduni, Utalii na masoko kupitia tasnia hiyo.

Hayo yamesemwa Mjini hapa hivi karibuni na Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk Herbert Makoye wakati wa mahafali ya 30, ambapo amesema kozi hizo zitasaidia kuongeza chachu ya ajira nchini.

Katika kuhakikisha Taasisi hiyo ya Sanaa na Utamaduni inafikia malengo yake na kupanua wigo mpana, Dk. Makoye alieleza ujio wa program hizo mbili mpya litafungua wigo mpana kwa Wasanii na watu mbalimbali watakao jitokeza kusoma kozi hizo.

“Tumeendelea na kuandaa programu mpya na hapo baadae tutakuwa na kozi za Astashahada na Stashahada.

Progamu ya kwanza ni ya Uongozi wa Sanaa na Masoko na pili ni ya Urithi wa Utamaduni na Utalii na hizi zimeshaandaliwa na zipo kwenye mchakato wa kupata Ithibati, kwa hiyo tukishapata na mwaka ujao wa masoko basi kozi zitaongezeka na taasisi yetu itasaidia kusonga mbele kwenye eneo la taaluma.” Alieleza Dk. Makoye.

Aidha, Dk. Makoye amefafanua kuwa, uwepo wa kozi hizo itakuwa chachu ya ukuaji wa masoko ya Sanaa hapa nchini hivyo ni wakati wa wadau kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo hapo baadae.

Pia aliwataka wahitimu hao wakawe wa mfano na wakakitangaze TaSUBa kwa mazuri waliyoyapata kwa muda wote waliokuwa chuoni hapo.

"Jumla ya wahitimu wote 148.  Kwa upande wa Stashahada Wanawake ni wanne (4),  na Wanaume 25. Kwa upande wa Astashaahda Wanawake 28, Wanaume 91. Ili ni ongezeko kubwa kutoka mwaka uliopita wahitimu nendeni mkawe mabalozi wazuri wa kuitangaza TaSUBa, alieleza Dk. Makoye.

Kwa pande wakem Mgeni rasmi katika Mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa amewapongeza wahitimu wote kwa kutimiza malemgo yao na kuweza kutunukiwa vyeti hivyo.

“Nawapongeza sana. Wahitimu wote kwa kuwatunuku vyeti na pia niwapongeze timu ya uongozi na wakufunzi wote wa wahitimu.
Taaluma inayotolewa hapa ni muhimu sana ndio maana Serikali yetu imeweka misingi imara ya taasisi hii” alieleza Zanaibu Kawawa.

Mgeni rasmi huyo pia amewapongeza uongozi wa TaSUBa kwa kuja na ujio wa kozi hizo mpya ambapo mchakato ukikamilika utakuwa na tija kubwa kutokana na kipaumbele cha Wilaya hiyo kuwa kitivo cha Sanaa na Utalii pamoja na Utamaduni.

“Mchakato huu wa ujio mpya wa kozi za Urithi wa Sanaa na Utalii na Sanaa na Masoko utakapokamilikautaleta tija kubwa kwa kuwa unaendana kabis na vipaumbele vyetu vya serikali ya Wilaya ya kuifanya Bagamoyo kuwa kitivo cha Utalii, kitivo cha Sanaa na kuwa kitivo cha Utamaduni” alimalizia, Zainabu Kawawa.

Kawawa pia amesema uzuri wa Bagamoyo imekuwa na fursa nyingi ikiwemo vivutuo vya Utalii vikielezea historia za makoloni karibu yote ambapo kumbukumbu zao bado zipo hapo mpaka leo hii.

TaSUBa  imekuwa ikifundisha elimu ya sanaa na utamaduni kwa kukuza na kuendeleza vipaji vya wasanii mbalimbali hapa nchini  huku wengi wakiwa na uhakika wa ajira na kuajiajiri na miongoni mwa wanaopata ajira ni pamoja na Maafisa Utamaduni na wakuu wa idara za Sanaa mashuleni na vyuoni ambao wengi wao wamepitia katika taasisi hiyo kongwe hapa nchini.
  Mgeni rasmi katika Mahafali ya 30 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Bi. Zainabu Kawawa akiwatunuku vyeti vya Astashahada na Shahada wahitimu mbalimbali wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika Desemba 7 mwaka huu. Mjini Bagamoyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...