Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa haki ya wakimbizi kurejea nchini mwao au kubaki kwa wakimbizi waishio nchini wakitokea Burundi itaendelea kuwepo na kuwa la hiari na hiyo ni pamoja na kupata  huduma za msingi ikiwepo ulinzi kwa wakimbizi watakaobakia nchini na kwa wale watakaorejea nchini mwao watahakikishiwa usalama wa kurejea nchini mwao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo amesema, kupitia kikao cha siku tatu cha mkutano wa 21 wa Tripartite commission kilichowakutanisha na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Kangi Lugola na wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi duniani (UNHCR) walipata wakati mzuri wa kujadili masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao.

"Wakimbizi kurejea Burundi ni hiari na watakaoamua  kurejea katika nchi zao tutashirikiana nao kwa Kuhakikisha wanarejea nchini mwao salama kabisa,  tutawafikisha kwenye mipaka ya nchi zao na wale watakao endelea kubaki nchini UNHCR kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Burundi tutaendelea kushirikiana nao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yote ya msingi" ameeleza Okoth -Obbo.

Pia amesema kuwa kupitia mkutano huo wamekubalina kuwa Tanzania iendele kutoa taarifa za wakimbizi hasa vyeti vya kuzaliwa, vifo na vyeti vya wakimbizi katika shirika la UNHCR.

"Taarifa zinazowahusu wakimbizi ni muhimu sana katika kuisaidia kutoa mahitaji ya msingi ni vyema Tanzania ikaendelea kutoa taarifa kupitia nyaraka mbalimbali zinazoonesha  ndoa, uzazi na vifo"

Amesema kuwa UNHCR Tanzania inahitaji dola za kimarekani 126 na kueleza kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakishiriki kwa namna moja au nyingine kwa Kuhakikisha wakimbizi hao wanapata huduma muhimu hasa zile za kijamii.

Okoth amesema kuwa  baada ya mkutano huo alitembelea kambi za Nduta na Mtendeli zilizopo Mkoani Kigoma ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na wakimbizi pamoja na viongozi na washiriki wanaohudumia wakimbizi katika nchi hizo.

" Niipongeze Serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa kubeba jukumu la kubeba wakimbizi wapatao 246,000 katika nchi yao na katika kambi nilizopita Kigoma nilipata kushuhudia wakimbizi wakijiandikisha kwa hiari ili wapate kurejea makwao." Ameeleza.

Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya wakimbizi wanatoka katika nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo huku 87 ya wakimbizi hao wakiishi katika kambi tatu zilizopo Mkoani Kigoma.
 Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar  kuhusu mambo mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye kikao chao cha siku tatu kilichowakutanisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Mhe.Kangi Lugola,Wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi Duniani (UNHCR),namna walivyojadili  masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao. 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza na  Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo,jana jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...